Thursday 22 June 2023

WATU 10 WAMEHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA JELA NA KUNYONGWA MPAKA KUFA BAADA YA KUPATIKANA NA HATIA KESI YA KUMUUA MLINZI WA OFISI YA KIJIJI KILINDI,,,,

Pichani ni Washtakiwa 10 ambao walishtakiwa kwa tuhuma za  ugaidi mara baada ya kuhukumiwa wakiwa kwenye gari ya polisi wakitoka mahakamani kuelekea gereza la Maweni lililopo nje kidogo na jiji la Tanga.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MAHAKAMA Kuu Kanda ya Tanga imewahukumu kifungo cha maisha na Kunyongwa hadi kufa washtakiwa 10 kwa kupatikana na hatia katika kosa la mauaji ya Marehemu Mbwana Salim  Kilo aliyekuwa mlinzi wa Ofisi ya Kijiji cha Lulago wilayani Kilindi Mkoani  Tanga.

Hukumu hiyo imetolwa na Jaji Mfawdhi wa Mahakama kuu kanda ya Tanga,Latifa Mansour baada ya kujiridhisha na ushahidi uliotolewa pande zote.

Kabla ya hukumu hiyo ilielezwa mahakamani hapo kwamba washtakiwa walidaiwa kutenda  kosa hilo October 10 mwaka 2013 huko katika kijini cha Lulago kilichopo wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga 

Akitoa hukumu hiyo Jaji Mansour alisema kwamba kutokana na ushahidi uliotolewa na pande zote mbili Mahakama imejiridhisha na kuwatia hatiani  ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.

''Nawahukumu kifungo cha maisha jela na kunyongwa hadi kufa chini ya kifungu cha 196 na 197 cha sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyo fanyiwa marejeo mwaka 2022'' Alisema Jaji Latifa. 

Waliohukumiwa hukumu hiyo ni Haji Omary Mzana, Khalid Salehe Sekinzu, Omary Said, Toba Salehe Sekinzu, Abdallah Mrisho, Mnyamisi Said, Abdulrahman Hassan, Juma Omary, Ramadhani Athuman Mnguu na Jawa Omari Mzana.

Awali katika kesi hiyo Washtakiwa walikua 20 ambao walishtakiwa kwa tuhuma za  ugaidi ambapo tisa kati yao waliachiwa huru baada ya kukosekana ushahidi na baadae Mashtaka yakabadilishwa na kuwa kesi ya mauaji ya namba 22 ya Mwaka 2022

Katika  hukumu hiyo iliyotolewa jana  mshtakiwa mmoja aliachiwa huru baada ya upande wa ushahidi kuonyesha kuwa ameshtakiwa kwa jina lisilokuwa lake.

Upande wa washtakiwa ulikuwa na mashahidi tisa wakati upande wa utetetzi walikua 20.
Mwisho.


Picha na Sophia Wakati,Tanga

No comments:

Post a Comment