Monday, 19 June 2023

CCM KOROGWE VIJIJINI JINSI ILIVYO WAJENGEA UWEZO WANACHAMA WAKE NA VIONGOZI,,

Pichani ni katibu wa CCM Halmashauri ya Korogwe vijijini,Fatma Shomari akielezea mpango mkakati wa kutoa mafunzo kwa wanachama wa chama cha mapinduzi wilayani hapo.

 NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi CCM Korogwe Vijijini, Fatma Shomari, amesema kwamba wanampango mkakati kutoa Semina elekezi kwa Watendaji hatua ambayo itawawezesha kutekeleza majumu yao kwa ufanisi.


Fatma ametoa taarifa hiyo ofisini kwake wakati akizungumza na Waandishi wa habari Wilayani Korogwe Mkoani Tanga kutaka kujua mpango wa kuwanoa wanachama.

Alisema,kwamba semina hiyo elekezi ni mpango madhubuti wa Chama tawala kuwapatia Viongozi wake kila baada ya miaka mitano (5) pindi wanapochaguliwa.

Aidha,alisema kuwa,semina hizo elekezi zitatolewa kwa viongozi wapya ambao ni makatibu wa Chama na jumuiya kwa ngazi za shina,tawi,kata na wilaya.

"Baada ya miaka mitano toka wapatikane viongozi wapya tuna utaratibu wa kutoa semina elekezi,hizi zinawasaidia kujua mipaka yao"alisema Shomari.

Katibu huyo pia amebainisha kuwa kama semena elekezi hazijatolewa inakuwa vigumu kuwadai taarifa viongozi hao wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aliongeza kusema kuwa, mchakato huo umeshaanza ambapo zoezi hilo la utolewaji semina elekezi litafanyika kwa kata zote 29 na matawi yaliopo Korogwe Vijijini.

Alisema, katika hatua ya kwanza kata zitakazohusika ni Hale, Mnyuzi, Magila Gereza, Makuyuni, Chekelei, Mazinde, Mombo na ile ya Mkomazi.

Kwa mujibu wa Fatma,alieleza semina elekeza itakwenda sambamba na upachikaji wa bendera kwenye mashina kwa Mabalozi.

Vilevile katiba na kanuni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) zitatolewa kwa viongozi hao kupitia utaratibu maalum uliopo ndani ya Chama hicho tawala.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment