Pichani mkono wa kulia ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Lushoto, Ally Daffa, akimpongezi Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Tanga,Henry Mwaibambe kuboresha utendaji wake kuwa karibu na Wananchi kuwatatulia kero zao za uhalifu.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI la Polisi Mkoani Tanga limeelezwa kufanikiwa kuboresha utendaji kazi wake kwa kuzingatia utendaji wenye weledi na uadilifu katika kuwahudumia Wananchi hatua ambayo ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Lushoto, Ally Daffa, ametoa Pongezi hizo Jana ambapo alitanabaisha kuwa kwa sasa Jeshi hilo limeboresha utendaji wake kutokana na kuwa karibu na Wananchi kuwatatulia kero zao za uhalifu.
Daffa alisema kwamba, katika matukio mbalimbali yanayotokea wilayani Lushoto, askari wa Jeshi la Polisi wamekuwa wakiwahi kufika maeneo yenye changamoto na hivyo kupunguza madhara zaidi kujitokeza kwa jamii.
"Nataka kusema ukweli, Polisi wilayani kwetu wanafanya kazi hapa Kamanda wa Jeshi hilo mkoa amekuwa akihangaika huku na huko kuhakikisha Mkoa unakuwa Salama bila kuwepo uhalifu"alisema Kiongozi huyo wa CCM Daffa.
Daffa alisema kuwa, ni jambo jema kwa mtu yeyote kupongezwa pindi anapofanya vizuri na ndio sababu amechukua hatua ya kulipongeza Jeshi la Polisi kwa jinsi linavyofanya kazi kwa weledi kukabiliana na matukio ya uhalifu kwa kuwahudumia vyema Wananchi.
"Wakifanya vyema tuwasifie, wakifanya vibaya tuwakosoe"alisema Mwenyekiti huyo wa CCM,Daffa aliyetunukiwa Cheti na Jeshi la Polisi cheti cha kusafishwa 'Police Clearance Certificate', ambacho mtu yeyote anatunukiwa baada ya kuchunguzwa na kuthibitishwa kuwa na tabia njema.
Mwenyekiti huyo wa CCM wilayani Lushoto,aliendelea kusema kuwa kwa jinsi Polisi wanavyofanya kazi vizuri ni dhahiri kwamba wanatekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kutokana na kutoa huduma bora kwa jamii iliyopo.
Daffa ametoa wito kwa Wananchi kushirikiana vyema na Jeshi la Polisi ili kuweza kudhibiti vitendo vya uhalifu huku akitumia fursa hiyo kuwasisitiza kuendelea kufanya kazi zao kwa udilifu.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment