Pichani ni miongoni mwa meli kubwa ambayo zimewasili bandari ya Tanga baada ya maboresho.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari TPA imewataka Wananchi hususani watumiaji wa Bandari kuitumia Bandari ya Tanga hatua ambayo itawawezesha kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi.
Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Peter Milanzi ametoa wito huo alipokuwa akizungumza na Wanahabari mara baada ya kufungwa kwa Maonesho ya kumi ya biashara na Utalii Mkoani Tanga.
Milanzi ambaye ni Afisa uhusiano wa Bandari ya Tanga alisema kuwa, Tanga ni lango la kiuchumi Afrika Mashariki kutokana na ukweli kwamba Bandari ni lango la biashara kitaifa na kimataifa.
Aidha,amewahakikishia Wateja wake pindi watakapoitumia Bandari hiyo ya Tanga watapata huduma bora wanazozitarajia katika viwango vinavyohitajika kwa jamii.
''Siri ya mafanikio Bandari imezaliwa upya,tunafanya mambo mengi katika viwango vya kimataifa ''alisema Kaimu huyo Meneja wa Bandari ya Tanga.
Kuhusu ushiriki wa Bandari katika Maonesho ya kumi ya biashara Kwa mwaka huu, alisema kwamba lengo lao ni kuhamasisha Wananchi na wafanyabishara kuitumia Bandari ya Tanga.
Aidha,alibainisha kwamba Bandari ya Tanga imefanyiwa maboresho makubwa katika mradi wa kimkakati uliotekelezwa na Serikali kupitia mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania.
Alisema,lengo la mradi huo ni kuiwezesha Bandari kuhudumia meli na mizigo mikubwa huku akubainisha kuwa hapo awali meli kubwa zilishindwa kuingia Bandarini na hivyo kuwa changamoto kwa wafanyabishara.
Alisema,kuwa utekelezwaji mradi huo unawezeaha meli kufika Bandarini na kuhudumiwa kwa haraka na kwa ufanisi mkubwa zaidi.
Naye Mkuu wa kitengo Cha masoko na biashara TPA Tanga, Rose Tandiko alisema wamefanikiwa kuongeza vifaa vipya vya kutosheleza huku ghati likiwa jipya na pia ari ya wafanyakazi ikiwa imeongezeka kwa kiwango Cha juu.
Alisema kuwa wafanyakazi waliopo wako tayari kuhudumia meli na mizigo ya aina mbalimbali ambapo alitoa wito Kwa wadau kuitumia Bandari ya Tanga.
Tandiko alisema, kupitia Maonesho ya kumi ya biashara Kwa mwaka huu wameweza kukutana na wadau wengi kujadiliana mambo mbalimbali ambapo watayafanyia kazi Kwa lengo la kubotesha shughuli zao za utendaji.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment