Sunday 2 July 2023

KIKAO CHA KUZIBA NAFASI ZA UONGOZI CHAMA CHA BODABODA WILAYA YA TANGA WADAU WAJITOKEZA KUTANGAZA FURSA MBALIMBALI,,,,



Pichani katikati ambaye amesimama ameshika kipaza sauti ni Mwenyekiti wa chama cha waendesha Bodaboda Wilaya ya Tanga,Mohamded Chande katika akiwa kwenye ukumbi wa YDCP mkutano maalum mara baada ya kuziba nafasi za tatu za uongozi akiwatambulisha wanachama uwepo wa wadau mbalimbali na kuwataka kuwasikiliza.

   NA SOPHIA WAKATI,TANGA
CHAMA Cha Waendesga Bodaboda Wilayani Tanga kimefanikiwa kupata Viongozi wake wapya watatu ambao ni Kaimu Katibu msaidizi,Kaimu Kamanda msaidizi na mjumbe wa chama hicho baada ya wale wa awali kutenda makosa yaliyoshindwa kuzuilika kwa mujibu wa Katiba.

Mwenyekiti wa Bodaboda Wilaya ya Tanga,Mohamded Chande alitoa taarifa hiyo juzi katika ukumbi wa YDCP mara baada ya mkutano wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga.

Alisema kuwa Viongozi wapya waliochaguliwa na Kamati tendaji kwenye kikao hicho ni Juma Goa ambaye ni Katibu msaidizi, Khalidi Shedangilo ambaye ni kamanda msaidizi wa bodaboda na Jafhet Lukuta mjumbe wa chama hicho.

Chande alisema kwamba, kamati tendaji ililazimika kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi baada ya viongozi waliokuwepo awali kufanya makosa ambapo Katiba yao inaruhusu kuchaguliwa kwa viongozi wengine bila hata ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa Chama huicho cha waendesha bodaboda wilayani Tanga.

"Ibara ya kumi 21, 2 kikatiba inasema, kamati itawaondoa na kupachika watu ama viongozi wengine bila hata ya kufanyika kwa mkutano mkuu"alisema Mwenyekiti huyo wa Bodaboda wilayani Tanga,Alisema Mohamed.

Chande amewashukuru Viongozi wa bodaboda kwenye vituo vyote kwa kufanikiwa kuziba nafasi hizo zilizoachwa wazi ambapo aliwasisitiza wanachama wa Chama chake kuzingatia sheria za usalama barabnarani.

Pamoja na hayo,Mwenyekiti Chande alisema kwamba, amefarijika Bodaboda kujiwa na fursa ya kukopeshwa Viwanja kwa bei ya shilingi 3,000 kwa siku hadi pale watakapokamilisha gharama halisi na kuweza kupatiwa hati za kuvimiliki.

"Tunamshukuru kupata mpango wa Daka Kiwanja kwa bei ya sh 3,000, hii itatusaidia sisi nbodaboda ambao ni wanyoinge"alisema Chande akiwasaihi wanachama wake kuwa tayari kunufaika na utaratibu huo wenye umuhimu.

Katika kikao hicho cha Bodaboda pia alikuwepo mwakilishi wa Kampuni ya uzalishaji na usambazaji  Oili ya Mogas ambaye aliwasihi Vijana wa bodaboda kutumia bidhaa wanazozalisha kwa kuwa ni rafiki wa mazingira.

Alibainisha zaidi akisema kuwa ubora wa bidhaa hizo zinazozalishwa na Mogas nzuri na bei yake ni nafuu kwa kutokana na shughuli zao.
Mwisho.  



Pichani mkono wa kushoto ni Afisa Masoko wa kampuni ya Mogas,Teodora Msingwa wakati akitoa ya ubora ya bidhaa yao Oil ya Mogas kwenye kikao cha waendesha bodaboda wa pikipiki na Bajaji wilayani Tanga na kuwataka kuitumia na kupunguza gharama.


NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WAZALISHAJI na wasambazaji wa Vilainishi aina ya Oil ya Mogas yenye makao yake makuu Jijini Tanga imewasihi waendesha Bodaboda kutumia mafuta wanayozalisha kwa vile gharama yake ni nafuu na pia yakiwa rafiki wa mazingira.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa masoko wa kampuni hiyo  ya Mogas,Teodora Msingwa juzi wakati akizungumza kwenye kikao cha waendesha bodaboda wa pikipiki na Bajaji wilayani Tanga.

Teodora alisema kwamba kwa kuthamini mchango wa wadau wa bodaboda, Kampuni ya Mogas imekuja na bidhaa bora aina ya Oil kwa ajili ya wateja wake.

Alisema, Oil wanayozalisha ina ubora wa hali ya juu akiieleza kulinda chombo atumiacho mwendesha wa bodaboda sambamba na kumuepusha kupata masilahi huku bidhaa hiyo ikisafisha injini.

"Kiukweli Oil yetu inasafisha injini , kuondoa kitu na pia ni rafiki wa mazingira. Tunawaomba waendesha bodaboda ambao bado hawajaanza kutumia bidhaa zetu wajaribu waone mafanikio"alisema Msingwa.

Akielezea zaidi,Teodora alisema Kampuni yao imeweka kiwanda Jijini Tanga huko eneo la Kisosora Jijini Tanga wakiwa wanazalisha Oil za magari makubwa na madogo pamoja na pikipiki na hata bajaji.

Hata hivyo, Kampuni hiyo ya Mogas imekuwa ikiuza bidhaa zake huko katika nchi za Ukanda,Rwandan,Burundi,Congo na hapa nyumbani Tanzania.
Mwisho.



Pichani mkono wa kushoto ambaye amevaa koti ni miongoni  mwa wafanyakazi wa kampuni ya Mogas akiwa katika mkutano akijibu na kuuza bidhaa hiyo. 

Pichani mkono wa kushoto  ambaye ameshika kipaza sauti anazungumza ni Msimaminzi Afisa kitengo cha Masoko Kampuni ya Realbiz Company Limited,Godwin Lyakurwaakiwa katika mkutano ulioshirikisha vijana wajasiriamali kilichofanyika kata ya Centro Jijini Tanga akiwata kuchangamkia fursa ya Buku tatu kiwanja kutimiza ndoto zao,

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WAJASIRIAMALI Wilaya ya Tanga wametakiwa kuchangamkia fursa ya kununua Viwanja vilivyopewa utaratibu maalum unaofahamika Kwa jina la mkopo wa Buku tatu hatua ambayo imeelezwa kuwa ni sehemu ya kujitengeneza Pesheni zao za Uzeeni.

Msimaminzi Afisa kitengo cha masoko Kampuni ya Realbiz Company Limited,Godwin Lyakurwa  aliyasema hayo katika mkutano ulioshirikisha vijana wajasiriamali kilichofanyika juzi kata ya Centro Jijini Tanga,

Alisema kuwa wajasiriliama wanapaswa kutengeneza maisha Yao ya baadaye Kwa kununua Viwanja vya mkopo unaofahamika kama Buku tatu ili kuweza kutikiza ndoto zao.

Godwin alisema, mkopo wa Buku tatu unatoa fursa Kwa wananch kulipa fedha kidogo kidogo hadi kumaliza gharama nzima za Kiwanja baada ya kujaza mkataba rafiki wa kisheria utakaohusisha pande mbili ambazo ni mnunuzi na Kampuni husika.

Kwa mujibu wa Godwin alisema Mkopo wa 'Buku tatu' ukimaanisha malipo ya Shilingi elfu tatu, mteja anaweza kulipa Shilingi 3,000 kila siku hadi kufika hatua ya kumiliki Kiwanja kilichopimwa na chenye hati.

"Ukija kwetu unajaza fomu ambayo mazingira mazuri yametengenezwa kwa pande zote mbili kwa maana ya mnunuzi na Kampuni yeti, kuna utaratibu wa kulipa elfu tatu kila siku,21,000 kwa wiki na 90,000 mwezi hadi utakapomaliza kulipa mkopo"alisema Godwin.

Aidha alisema kwamba,iwapo kutatokea changamoto kwa mnunuzi na akahitaji kurejeshewa fedha zake ziko taratibu za kufuatwa Ili kupata haki yake ingawa kuna gharama za mtandao zitalazimika kukatwa katika huduma.

''Mkopo huo maarufu wa 'Buku tatu' imeelezwa kuwa Mkombozi Kwa Wajasiriamali hao wa Bodaboda ambapo wadau wa Tanga Mjini wamehamasishwa kuwahi fursa hiyo ya Viwanja vilivyopo mradi wa Pongwe''alisema Afisa masoko huyo Godwin.

Afisa ameeleza fursa zinazopatikana katika eneo hilo la Pongwe kuwa ni pamoja na uwepo wa Viwanja vyenye vipimo stahiki sanjari na kuzungukwa na Viwanda mbalimbali.

Pia aliwatoa hofu Wajasiriamali hao kwa kununua Viwanja vya Pongwe watapata uhalali wa kumiliki kisheria na hata ikitokea hitaji la Serikali kuendeleza eneo husika ni lazina mnunuzi atashirikishwa na kufidiwa.

Naye Mkurugenzi wa Kampuni  Realbiz Company Limited,Mahfudh Rubeya  alisema,kwamba lengo ni kuwawezesha wananch kumiliki maeneo na umuhimu mkubwa kwa mtu kununua kiwanja kwenye Kampuni kwa vile taratibu zote za kisheria zinafuatwa na hivyo ni rahisi kuepuka kujiingiza kwenye migogoro isiyo msingi.

Miongoni mwa wajasiliama wa soko la Uzunguni Dua Ally  alishukuru serikal na halmashauri ya jiji la Tanga kwa kutengeneza mazingira mazuri kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza jijini hapo.

Pia alitumia nafasi hiyo aliwasihi Vijana wenzake kuona umuhimu wa kuchangamkia fursa hiyo hatua ambayo itawapusha kuishi maisha ya kubahatisha akitanaisha kuwa wakati muafaka umefika kila mwanajumuiya wao kumiliki Makazi.
Mwisho


Pichani ni miongoni mwa viongozi na wafanyakazi wa kampuni ya Realbiz Company Limited,wakiwa katika mkutano huo wakisubiri kutoa elimu kwa wajasiliamali waendesha bodaboda ya bajaji na pikipiki jijini Tanga.

 

No comments:

Post a Comment