Saturday 15 July 2023

TIMU ISHIRINI ZAJITOKEZA KUWANIA ZAWADI ZA MASHINDANO YA ULINZI CUP 2023,,,,

Pichani mkono wa kulia aliyeshika kipaza sauti ni Meya wa Halmashauri ya jiji la Tanga,Abdurahaman Shiloo akifungua mashindano ya mpira wa miguu ya Ulinzi Cup 202 uwanja wa soka Magomeni aliwataka wazazi na walezi kushirikiana na jeshi la polisi katka kuwafichua watoto wanaojiusisha na tabia za uhalifu wa pili ni Diwani kata ya Duga na Jafari Mohame na akifuatiwa na Diwani kata ya Mabawa Athuman Babu.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

MICHUANO ya Soka kuwania Kombe la Ulinzi Cup 2023 imeanza kutimua Vumbi katika Uwanja wa soka Magomeni Jijini Tanga kwa kuzikutanisha timu za Edo Combine na Magomeni Star wenyeji uwanjani hapo, mchezo wa ufunguzi uliokuwa wa vuta ni kuvute hadi ukapelekea kupigwa kwa penalti na kuifanya Edoe Combine kuibuka kidedea kwa Penati 4-3.

Ligi hiyo inayokwenda kwa mtindo wa mtoano, Edo Combine walishinda kwa penalti nne kwa tatu,zile za washindi zilifungwa na Hatibu Mbaraka, Hamza Haruna, Athumani Kimath na Salimu Jumanne zile za Magomeni Star zilifungwa na Rajabu Mkamba, Swalehe Mohamed na Yohana Ngushi.

Mwamuzi wa katikati wa mchezo huo Peter Elias alionekana kuumudu vyema mchezo huo uliokuwa wa ufunguzi ambapo mgeni rasmi alikuwa Meya wa halmashauri ya Jiji la Tanga, Abdarahman Shiloo aliyewataka Vijana kutojihusisha na vitendo viovu hususani uhalifu, aliwataka kushirikiana na Polisi kuwafichua waliotaka kubadilika.

Meya huyo amempongeza Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe, kwa kuifanya michezo hiyo kuwa endelevu lengo likiwa kuwashirikisha na kuwa karibu na Vijana kupambana na vitendo vya uhalifu hatua ambayo pia ameieleza kuwa itaweza kusaidia katika kulifanya Jiji la Tanga kuendelea kuwa Salama wakati wote.

“Tuhakikishe wasio na tabia nzuri tunawaasa, wasiokubali kubadilika tushirikiane na Polisi katika kuwapatia taarifa” alisema Meya Shiloo huku akiendelea kuwaasa Vijana hao kuzingatia Sheria za nchi kwa kusisitiza suala la kuzingatia sheria za Usalama barabarani pindi wanapoendesha Bodaboda.

Vile vile Meya Shiloo aliwataka wazazi kuhakikisha kwamba Vijana wao hawazururi ovyo kuzidi muda wa saa sita za usiku kwa kisingizio cha kwenda kwenye muziki , aliwasihi kushauriana na watoto wao juu ya matembezi salama nyakati za hizo, pia alitumia fursa hiyo kuasa upigwaji  muziki kuzidi saa sita usiku.

Aidha Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tanga, Henry Mwaibambe aliwataka Vijana kuzingatia kuwa Ulinzi na Usalama ni suala linalowahusu watu wote pia aliwasihi kutojihusisha na vitendo vya kihalifu, aamewashauri Vijana hao kutumia michezo kujenga afya eneo ambalo pia huwatia ajira.

“Tucheze kwa furaha na amani, tulinde na kuendeleza vipaji vyetu kwa kuwa michezo sasa ni ajira”alisema Mwaibambe huku akiwasihi Wachezaji wa Magomeni Star na Edo Combine kutokubali kushawishika kuingia kwenye vitendo viovu vitakavyowatia matatani baada ya kukiuka sheria za nchi.

Mashindano hayo ambayo yanasimamiwa na SN Wakati Sports Promoters kwa kusirikiana na Dawati la Polisi jamii mkoa wa Tanga ambao waratibu wa Mashindano hayo ya Ulinzi Cup 2023 yenye lengo la kutoa elimu kwa Jamii hususani Vijana ili kuwawezesha kujikinga na vitendo vya uhalifu kama vile wizi, utumiaji wa dawa za kulevya, ukabaji na ubakaji na hata kuepuka unyanyasaji wa kijinsia.

Mwisho.


Pichani Katikatiamevaa fulana nyeupe ni Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe akiikagua timu ya Edoe Combine yenye maskani yake Mwakidila jijini Tanga wakati wa ufunguzi.


Pichani ni Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Tanga,Henry Mwaibamde akiwata vijana kuyatumia mashindano hayo kujenga urafiki na kushirikia kutoa taarifa za kuwafichua wahalifu katika maskani zao.


Pichani ambaye amevaa sare ya polisi ni Mratibu kutoka Dawati la Polisi jamii mkoa wa Tanga,Frank Kipengele akitoa elimu kwa vijana akiwataka kuyatumia mashindano hayo kutoa elimu ya kupinga uhalifu mkoani hapo na kuwa mabalozi  mkono wa kulia ni Promoter wa mashindano hayo kutoka ofisi ya SN Wakati General Promoter inayojihusisha na kuendeleza na kulea vipaji mbalimbali mkoani Tanga.

 NA SOPHIA WAKATI, TANGA

TIMU ya Soka ya Sigasiga FC jana imefanikiwa kuwabambiza Mabawa Polisi kwa kuwafunga magoli 3 – 1 katika mchezo wa kuwania Kombe la Ulinzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kombezi iliyopo Halmashauri ya Jiji la Tanga.

 

Kwa matokeo hayo sasa, Mabawa Polisi wameyaaga mashindano hayo ya Ulinzi Cup yanayoendelea kufanyika Uwanja huo wa Kombezi kwa mtindo wa mtoano, lengo la michezo hiyo ni jeshi la Polisi kuishirikisha Jamii kwenye masuala ya ulinzi na usalama.

 

Sigasiga ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao kwa njia ya penati kupitia kwa Rashidi Kitiwa, bao la pili lilifungwa na Ally Ramadhani baada ya kutokea piga ni kupige langoni mwa wapinzani wao na  lile la tatu lilifungwa na Abushiri Athumani kwa njia ya penati.

 

Goli la kufutia machozi la Mabawa Polisi lilifungwa kwa njia ya penati na Fredy Boflo na hadi mchezo huo ulipomalizika Sigasiga waliweza kuibuka kidedea huku Mabawa Polisi wakilazimika kufunga virago kwa maana ya kuiaga michuano hiyo ya Ulinzi Cup.

 

George Bakari Kyando alikuwa Mwamuzi wa kati katika mtanange huo alionekana kuumudu vyema huku akishirikiana na mshika kibendera namba moja Abdallah Mwabindo na Amiri Ismail ambao waliufanya mchezo kumalizikka kwa amani.

 

Awali kabla ya Timu hizo kuanza kumenyana, maafisa wa Jeshi la Polisi kitengo cha Usalama barabarani walitoa elimu kwa Vijana wote waliohudhuria Uwanjani hapo kushuhudia mchezo huo, waliaswa kuzingatia sheria ili amani kuendelea kuimarika.

 

Maafisa hao wa Polisi, walisisitiza suala la matumizi ya Kofia ngumu kwa Bodaboda, upatikanaji wa mafunzo na leseni sanjari na kuepuka vitendo vyote vilivyo hatarishi pindi wanapoendesha vyombo hivyo vya moto lengo likiwa kuepusha ajali.

 

Pamoja na hayo jamii imeaswa kutoa ushirikiano kwa jeshi la Polisi kwa kufichua uhalifu na vitendo vya uhalifu pindi vinapotokea, huku vijana wakiaswa kutojihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ama vitendo vyovyote ambavyo ni kinyume na sheria.

Mwisho.


No comments:

Post a Comment