Friday, 28 February 2025

TAKUKURU TANGA,JINSI ILIVYOFANIKIWA KUOKOA FEDHA ZA SERIKAL SH. 79,048,459.21 BAADA YA KUWAPANDISHA WATUMISHI MAHAKAMANI,,,

 Picha ni Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga,Ramadhani Ndwatah akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu watumishi ambao waliamriwa na Mahakama kurejesha fedha za Serikali mbali na kupewa adhabu nyingine ni kutoka wilaya tatu za Kilindi, Korogwe na wilaya ya Tanga Jiji, .

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TAASISI ya kuzuia na Kupambana na rushwa TAKUKURU Mkoani Tanga, imefanikiwa kuokoa fedha za Serikali Shilingi 76,048,459.21 baada ya kuwaburuza Mahakamani kwa ubadhilifu na ufujaji Mali za umma baadhi ya watumishi wasio waadilifu.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini  Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga,Ramadhani Ndwatah alisema kuwa watumishi hao ambao kwa amri ya Mahakama waliamriwa kurejesha fedha hizo za Serikali mbali na kupewa adhabu nyingine ni kutoka wilaya za Kilindi, Korogwe na wilaya ya Tanga Jiji, .

Ndwatah alisema kwamba, huko wilayani Kilindi Jamhuri ilishinda kesi ya uhujumu uchumi namba 13/2023, 11/2023 na 06/2024 dhidi ya watumishi walioshitakiwa kwa ubadhilifu kufuatia kutowasilisha mapato ya Serikali,fedha ambazo zilikusanywa kwa mfumo wa POS na kuzitumia kwa manufaa yao binafsi.

Akizungumzia zaidi alisema kwamba amri ya Mahakama,watumishi hao waliamriwa kurejesha Shilingi 58,678,780.00 sambamba na adhabu nyingine kutoka na kesi hiyo ya Jamhuri iliyokuwa ikiwakabili.

Kwa wilaya ya Korogwe kiasi cha Shilingi 9,198,045.35 ikiwa ni mapato ya Serikali yaliyokusanywa kwa POS pia yalirejeshwa kwa amri ya Mahakama katika kesi ya uhujumu uchumi namba 09/2023 na 10/2023.

Pia Jiji la Tanga Jamhuri ilishinda kesi ya uhujumu uchumi katika kesi namba 16558/2025 na 07/2023 ambapo jumla ya Shilingi 3,171,633.9 zilizofanywa ubadhilifu kwenye utekelezaji miradi ya maendeleo sekta ya elimu na 5,000,000.000 za mikopo ya asilimia kumi 10% za Wanawake,Vijana na walemavu zilirejeshwa.

Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoani Tanga,Ramadhani Ndwatah ametumia nafasi hiyo  kutoa onyo Kali kwa baadhi ya watumishi wenye tabia na fikra za kuhujumu rasilimali za umma kuacha mara moja tabia hiyo badala yake amewataka kuzingatia maadili na kanuni za kazi.

Vilevile Mkuu huyo wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga,amewataka wadau kuendelea kutekeleza Kauli mbiu isemayo "Kuzuia rushwa ni jukumu lako na langu; Tutimize wajibu wetu"huku akisisitiza kila mmoja Kuzuia vitendo vya rushwa.

Pia amewataka wadau kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kwenye ofisi yeyote ya TAKUKURU iliyo karibu na kila nwananchi au kupiga simu selula kwa namba za bure akitaja 113.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment