Friday, 20 June 2014

KAMATI YA UKIMWI KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI YAKUTANO KWA LENGO LA KUTOKOMEZA MAAMBUKIZI MAPYA NA KUFIKIA MALENGO YA SIFURI TATU.

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga   Ramadhani  Diliwa akifungua mkutano wa kamati ya ukimwi wilayani humo alipokuwa mgeni rasmi huku akieleza kuwa  maambukizi hayo yanaweza kuepukika kwa kuacha tabia za mchepuko kwa pande zote mbili  na kuwa waaminifu katika ndoa na kuepuka vishawishi ambapo asilimia kubwa ya maambukizi hayo wilayani humo yameelezwa ni kutokana na kuwepo kwa vitendo vya ngono zisizo salama . 

Kamati ya ukimwi katika halmashauri ya wilaya ya Handeni mkoani Tanga imekutana katika mkutano wa pamoja kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali  ambazo zinaweza kuondoka na kufikia malengo ya sifuri tatu.

No comments:

Post a Comment