Friday, 26 December 2014

FAINAL YA MASHINDANO YA NSSF CUP 2014 KADA YA WANAWAKE ILIKUWA HIVI,

 Timu ya kuvuta kamba ya wanawake Taswa Tanga Fc inayoundwa na waandishi wa habari,watangazaji wa redio na TV wakimsikiliza meneja wa NSSF Tanga ambaye hayupo pichani mara baada ya kumaliza kuvuta kamba na timu ya Vendas Fc uliofanyika uwanja wa Mkwakwani jijini hapo.
 Timu ya Vendas Fc ya mpira wa miguu,kufukuza kuku na kuvuta kamba wakimsikiliza meneja wa NSSF Tanga siku ya fainal.
 Mkono wa kushoto aliyevaa fulana nyekundu mwanaume ni meneja wa ofisi ya Wakati Sports Promoter,Fredrick Sospeter siku ya fainal hiyo akiwatangaza washindi wa mchezo wa kuku,kamba,mpira wa miguu ili kukabidhiwa zawadi na mgeni rasmi meneja wa NSSF Tanga,Frank Maduga.
 Meneja wa mfuko wa hifadhi ya jamii NSSF Tanga,Frank Maduga akimkagua kuku aliyeshindaniwa na kada ya wanawake siku ya fainal kabla ya kukabidhi zawadi hiyo.
 Mkono wa kulia ni mchezaji wa timu ya Vendas Fc wa mchezo wa kamba mara baada ya kukabiziwa baada ya kushinda kwa upande wa wanawake.
 Mkono wa kushoto ni meneja wa NSSF Tanga,Frank Maduga akimkabizi mchezaji wa timu ya Vendas Fc kwa upande wa wanaume kuku baada yakushinda,ambapo kwa upande wa kufukuza kuku wote walikwenda timu ya Vendas wa Tanga.
 Meneja akimkabidhi zawadi ya mpira kapten wa timu ya Macechu Sekondari ya wanawake baada ya kushika nafasi ya pili katika fainali hiyo.
 Meneja wa NSSF Tanga akimkabidhi zawadi ya seti ya jezi kapteni wa timu ya Usagara Fc ya wanawake baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya NSSF CUP 2014 kwa kufadhiliwa na mfuko huo.
Meneja wa NSSF mkoa wa Tanga akiwapongeza wachezaji na kuahidi kuendelea kudhami ili yaweze kufanyika kila mwaka kwani michezo ni ajira na kuishukuru ofisi ya Wakati Sports Promoter kwa kuyaratibu mashindano hayo ambayo yamekuwa ya kwanza kufanyika mkoani hapo.

No comments:

Post a Comment