Tuesday 28 March 2017

KAMANDA WA POLISI MKOANI TANGA,WAKULYAMBA,, AKISOMA TAARIFA YA OPERESHENI KATIKA BANDARI BUBU KIGOMBE WILAYANI MUHEZA,NA BABA ALIYEKINYUNGA KICHANGA KWA WIVU WA KIMAPENZI,,

 Pichani ni kamanda wa polisi mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba akisoma taarifa baada ya operesheni iliyofanyika katika bandari bubu ya kigombe wilayani Muheza.


NA SOPHIA WAKATI.TANGA
SHEHENA za bidhaa za magendo zikiwemo Sukari,mafuta ya kula na mchele zimekamatwa na jeshi la Polisi mkoani Tanga zikiwa zikekamatwa zikiwa zinateremshwa kwenye Bandari Bubu ya Kigombe iliyopo huko wilayani Muheza huku wamiliki wake wakiwa wanaendelea kusakwa ili hatua stahiki kuchukuliwa.

Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Benedict Wakulyamba alitoa taarifa hiyo jana wakati alipokuwa akizunbgumza na Gazeti hili huku akibainisha kuwa miongoni mwa bidhaa hizo za magendo zilizokamatwa kuna Sukari mifuko 64,mafuta ya kula aina ya OKI madumu 364 na mchele mifuko 10.

Kamanda wa Kulyamba alisema sukari hiyo ni ile ya kutoka nchini Brazili wakati mchele ukiwa umetoka Pakistani na mafuta ya kula yametoka Indonesia ambapo bidhaa hizo zote zilikuwa zimepakiwa kwenye Jahazi lenye nambari Z 1221 MV linalotambulika kwa jina la YARAZAKI huku mmiliki akikosa kujulinaka.

Alisema kuwa polisi kwa kushirikiana na maafisa wa TRA,Uvuvi doria waliweza kukikamata chombo hicho kilichokuwa na bidhaa hizo za magendo huko bandari Bubu ya Kigombe kata ya Kigombe wilayani Muheza ambapo bado mpaka sasa thamani halisi ya vitu vinavyoshikiliwa haijaweza kufahamika.

Aidha kamanda Wakulyamba alisema kuwa jeshi la polisi linaendelea kumsaka Nahonda wa Jahazi hilo mmiliki wa chombo na mwenye bidhaa ambazo zilikuwa zikisafirishwa huku akifafanua kuwa mifuko 10 ya mchele uzito wake kila mmoja ilikuwa kilogramu 50,sukari kila mmoja kilogramu 50 na hayo mafuta.

“Tunaendelea kuwasaka wale wote wanaohusika na kusafirisha mzigo huo wa magendo ambapo mpaka sasa hatujafanikiwa kuwanasa,tunamtafuta Nahodha,mmiliki wa chombo na hata mwenye mzigo ambao ulikuwa ukisafirishwa ili hatua za kisheria kuweza kuchukuluiwa”alisema kamanda Wakulyamba.

Ametoa wito kwa wafanyabiashara kufuata mfumo rasmi ili kulipa kodi kwa ustawi wan chi yetu huku akiasa tabia za baadhi ya wafanyabiashara kujihusisha na magendo jambo ambalo kisheria halikubaliki ambapo linaweza kumsababishia mshiriki wa shughuli hiyo kupatwa na matatizo yasiyo na msingi.
Mwisho. 



NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
JESHI la polisi wilayani Korogwe mkoani Tanga,liko kwenye opresheni kumsaka mkazi mmoja wa Magunga wilayani hapo,Ibrahim Kichele (40)kwa tuhuma za kumnyonga kichanga cha miezi minne Ramadhan Ibrahim na kumtupa porini kwa kile kilichodaiwa ugomvi wa kifamilia na wivu wa kimapenzi.

Hata hivyo,habari ambazo sio rasmi zilieleza kwamba chanzo cha ugomvi huo ni Ibrahim Kichele alipata taarifa kutoka nje kwa majirani kwamba kichanga hicho sio mtoto wake chake.

Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba akidhibitisha alisema tukio hilo limetokea juzi saa 8.00 usiku huko katika kijiji cha Kwasamangube kilichopo wilayani Korogwe.

Alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa Ibrahim Kichele alikwenda nyumbani kwa mama mkwe wake alikokuwa akiishi mtaraka wake aliyefahamika kwa jina la Hadija Kitigo (26) ambaye walitengana mwaka mmoja uliopita.

Kamanda Wakulyamba alisema baada ya kufika kwa mkwewe huyo kugonga na kuingia ndani kwenye chumba alichokuwa akiishi mtaraka wake ambaye alizaa nae watoto wawili.

“Baada ya kuingia ndani ya chumba alichokuwa akiishi mtaraka wake Hadija mara kulizuka ugomvi uliopelekea kumchoma kisu  sehemu ya shavu na mkono wa kulia na kuondoka na kichanga kutokomea nacho kusiko julikana”alisema.

Kamanda Wakulyamba alisema maiti kichanga hicho ilipatatika March mosi,mwaka huu mchana katika kichaka huku kikiwa kimeuwawa kwa kunyongwa na kubamizwa kwenye fuvu lake la kichwa.

Aidha alisema taarifa za tukio hilo ziliwasilishwa kituo cha polisi wilayani Korogwe na uongozi wa kijiji hicho cha Kwasamangube Magunga wilayani hapo.

Alibainisha kwamba polisi walifika eneo la tukio na kumkuta mwanamke huyo akiwa amelala chini huku akijiuguza ambapo walimchukua na kumkimbiza hospital ya Magunga kwa matibabu na kufanya msako katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza na Uhuru,Aziza Ramadhani ambaye ni mama mkwe wa Hadija alisema mkwe wake alifika nyumbani kwake mapema kama ilivyo desturi yake ya kwenda kumbembeleza mkewe kwa lengo la kurudiana na kuwajulia hali watoto wake ndipo kuzuka kwa vurugu hizo.
Mwisho.

​Pichani ni kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba jana akizungumzia sakata la mkazi wa Kwasamangube Kichele aliyemcharanga mtaraka wake mapanga na kutokomea na kichanga cha miezi 4 kutimiza lengo lake la kukinyonga kwa wivu wa kimapenzi.

No comments:

Post a Comment