Sunday 2 April 2017

ALIYEKUWA MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA MUHEZA AKIELEZA SABABU ZA KUJITOA KWENYE CHAMA HICHO,,,

Pichani aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo wilayani Muheza,,Rwebangira Mathias Kharuasha akizungumza na waandishi wa habari mkoani Tanga sababu za kujitoa kwenye chama hicho.
 
NA SOPHIA WAKATI,MUHEZA
MWENYEKITI wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA wilayani Muheza,Rwebangira Mathias Kharuasha amejiengua chama hicho kwa kile alichoeleza kuwa ni kutokana na kuchoshwa na sera mbovu za chama hicho.

Hata hivyo amesema sababu nyingine likiwemo suala la mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA,Freeman Mbowe kushiriki utoaji maneno ya kashfa dhidi ya Rais Dk.John Magufuli  ambaye amekuwa mkombozi katika uongozi wake kuinusuru nchi
,alipokuwa ziara yake hivi karibuni mkoani Tanga.


Rwebangira alitoa taarifa hiyo jana alipokuwa akitangaza kujiuzulu mbele ya waandishi wa habari ambapo alisema kuwa amejiondoa kundini baada ya kutoridhishwa na mwenendo mzima wa chama hicho kwa viongozi wake wakuu kukosa dira,kirimu na maendeleo huku wakidiriki kukiuka makubaliano zao wakizikana kauli zao.


Mwenyekiti huyo aliyejiengua alisema,ameshangazwa na mwenyekiti wake huyo wa Taifa kusema kuwa hata siku moja haitatokea wao kuchukua mwanachama kutoka CCM na badala yake amelamba matapishi kwa kuwakaribisha kwenye chama mawaziri wakuu wastaafu Edward Lowassa na Frederick Sumaye.


Mbali na hao Rwebangira alisema,hivi sasa wapo wanachama wengi waliofukuzwa CCM wamechukuliwa na chama hicho wakati awali kupitia mwenyekiti huo,Mbowe na viongozi wengine waaandamizi wa CHADEMA walijinadi kwamba hawawezi kuwachukua wanachama wa aina hiyo wakiwafananisha na matapishi.


Alisema,anashangazwa kuona kuwa CHADEMA ina viongozi wengi waliokuwa na elimu ya vyuo vikuu lakini wameshindwa kumshauri mwenyekiti wao wa Taifa hatua ambayo imemfikisha mahali amekuwa akitoa maneno ya kashfa ambayo wakati mwingine amekuwa akishindwa kusimamia hoja zake ndani ya chama hicho.

"Chadema inawasomi wengi kutoka vyuo vikuu mbalimbali lakini hawajui historia ya nchi,mimi kuanzia mwaka 1959 ni miongoni mwa waasisi ambao wameipigania nchi hii kupata ukombozi enzi za Tanu hivyo naijua vizuri nchi"alisema.


Kutokana na hayo yote Rwebangira alisema kwamba ameamua kujiondoa kwenye chama hicho na kurejea CCM akiamini kuwa huko ndiko anakoweza kutoa mchango wake na kuiletea tija jamii badala ya kuendelea kubaki upande ambapo umepoteza dira na mwelekeo katika mustakabali wa kuijenga nchi.


“Mbowe na wenzake tena wa ngazi ya Taifa wanashangaza,walisema kwamba hawawezi kuchukua wale wanaohama kutoka CCM wakiwaita kuwa matapishi sasa imekuaje kuwachukua Lowassa na Sumaye na wengine wengi tu,kauli zao zinawachanganya wananchi pia waache kutoa kashfa kwa Rais Dk.Magufuli juu ya utendaji wake”alisema.


Aidha,pia amemmwagia sifa Dk.John Magufuli kwamba ni kiongozi ambaye ameonyesha uwezo mkubwa katika kuwatumikia watanzania ambapo anapaswa kupewa wasaa wa kuendelea kuwajibika kwa uadilifu huku akiasa tabia za baadhi ya wapinzania kuzusha maneno yasiyo na msingi kuichanganya jamii.


Alisema kuwa baada ya kuamua kuchukua uamuzi wake huo kujiwengua katika chama hicho kuanzia sasa yuko tayari kuitumikia CCM kwa nafasi yeyote ile atakayopewa ambapo amekiri kuwa ni CCM pekee itakayoweza kuivusha Tanzania hapa ilipo kutoka sehemu moja kwenda nyingine akiwasihi wananchi kuendelea kukipa ridhaa chama hicho.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment