Monday 17 April 2017

KANISA LA SABATO KANA JIJINI TANGA IMETUMIA SHEREHE ZA PASAKA KULAANI VITENDO VYA MAUAJI YA POLISI KIBITI NA KUMUUNGA MKONO RAIS DK.JOHN MAGUFULI KUFANYA KAZI ZA KIJAMII NA MADHEHEBU MENGINE,,,

 Pichani ni mchungaji wa kanisa la Sabato,Jackson akifuatilia waumini wa madhehebu ya dini mbalimbali na askari wa jeshi la polisi mkoani Tanga wakiwa katika kazi za kijamii eneo la Uhuru Park miaka 21.
 Pichani ni Mchungaji wa kanisa la Sabato Kana jijini Tang,Jackson Gladson akizungumza na waandishi wa habari (ambao hawako pichani)lengo la kuungana na madhehebu mengine kufanya kazi za kijamii eneo la Uhuru Park miaka 21 jijini Tanga.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KANISA la Sabato lililopo Kana Jijini Tanga limeshirikana na jeshi la Polisi kuimarisha Usafi wa mazingira huku Mchungaji wa kanisa hilo,Jackson Gladson akisema kufanya hivyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk.John  Magufili katika utendaji kazi wake huku mahusiano yakiimarishwa na vyombo vya ulinzi na usalama.
Mchungaji Gladson alisema wameamua kutumia siku hiyo ya kusherehekea sikukuu ya Pasaka kuimarisha usafi wa mazingira kwa kushirikiana na jeshi la polisi wakiamini kuwa ni njia mojawapo ya kuimarisha mahusiano sanjari na kuboresha afya ya jamii.
Aidha, alisema kwamba,wameamua kuitumia siku hiyo kuungana na polisi kuwakumbuka na kuomboleza dhidi ya askari waliouawa kikatili na majambazi huko Kibiti vitendo ambavyo alisema vinapaswa kulaaniwa vikali miongoni mwa jamii ya watanzania.
Alisema,kanisa kama waumini na jamii nzima wanapaswa kuungana na polisi kwenye kipindi hiki kigumu kuonyesha Uzalendo wa kweli huku akiahidi kusema kuwa mahusiano yao na jeshi la polisi yatakuwa endelevu.
"Neno la Mungu linatuagiza kwamba tumtangulize mbele Mungu katika kazi zetu zote hata zile za mikono kwa hiyo tumeamua tuitumie siku hii kufanya kazi za mikono huku tukishirikiana na polisi"alisema Mchungaji.
Kwa upande wake kamanda wa polisi mkoani Tanga Benedict Wakulyamba alimpongeza mchungaji huyo kwa hatua yake ya kuwaunganisha wakristo na jeshi la polisi akisema hilo litasaidia kudumisha amani na utulivu miongoni mwa jamii ya wana Tanga.
Alisema kwamba utaratibu huyo ni sehemu ya falsafa ambayo imeachwa na Baba wa Taifa mwalimu Julius Nyrere ambayo inapaswa kuenziwa na watanzania wote mazingira ambayo yanalenga kudumisha amani na utulivu.
Naye afisa afya wa Jiji la Tanga,Kizito Nkwabi alisema kwamba kuna haja ya jamii kuimarisha usafi kwenye mazingira yake hatua ambayo itaiwezesha kuepkana na magonjwa yanayoweza kuepukika kirahisi ikiwemo yale ya miripuko.
Mwisho.
  Pichani ni kamanda wa polisi mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba mara baada ya kushiriki zoezi la usafi eneo la Uhuru Park miaka 21,jiji hapo akimpongeza mchungaji wa kanisa la Sabato Kana Jackson kwa hatua yake ya kuwaunganisha wakristo,madhehebu mengine ya dini na jeshi la polisi amesema mpango huo utasaidia kudumisha amani na utulivu miongoni mwa jamii ya wana Tanga.
 Baadhi ya waumini wakifanya usafi.
 Picha ni gari la kuondosha takataka lililotolewa na halmashauri ya jiji la Tanga liondosha uchafu.
 Pichani ni miongoni mwa waumini wa madhehebu ya dini wakiendelea na zoezi la kugawa vitabu vya dini vyenye maelekezo ya mungu katika eneo hilo la Uhuru Park maarufu miaka 21 jijini Tanga.
Pichani ni waumini wa kanisa la Sabato Kana jijini Tanga wakisubiri kukusanya majani yanayofyekwa.

No comments:

Post a Comment