Friday 23 June 2017

RPC TANGA,WAKULYAMBA APIGA MARUFUKU DISKO TOTO NA WATU KUOGELEA FUKWE AMBAZO SIO RASMI EID ELFITRI MKOANI HAPO,,

 Pichani ni kamanda wa polisi mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba akizungumza na waandishi wa habari hawako pichani kuelekea s/kuu ya Eid elfitri ,

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI la polisi mkoaniTanga,limepiga marufuku watu wanaojiandaa kuendesha disko toto katika kumbi mbalimbali za starehe wakati huu wa kuelekea sikukuu ya Eid elFitri mkoani hapo,huku likiwataka waache kufanya hivyo vinginevyo watachukuliwa hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake,Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba, alisema kuwa jeshi lake limejipanga kuweka ulinzi katika maeneo ya kumbi za starehe, nyumba za ibada pamoja na fukwe za bahari wakati huu wa sikukuu.

TumetoamaelekezokwawananchiwetuwotemkoaniTanga, kwambatumepigamarufukukuendeshadisko Toto katikamaeneoyoteyamkoa,anayefanyamaandaliziaachemaramoja, mambo hayonikinyume cha maadili yetu lakini pia ni kinyume cha sheria,”alisemaKamandahuyo.

Pia kamanda huyo wa polisi alisema kuwa ni marufuku kwa watoto kukutwa wakiogelea bila ya kuwa na wazazi au walezi watakaowaangalia katika sikukuu na kwamba kufanya hivyo wakikutwa wazazi ndiyo watawajibika kwa kushitaki kwa vyombo vya kisheria.

Kamanda huyo alisema pamoja na watoto kukatazwa kuogelea lakini pia watu wazima wametakiwa waache mara moja kwenda kuogelea katika maeneo ambayo hayajatengwa rasmi kwa watu kuogelea na badala yake wakaogelee katika maeneo maalum yanayojulikana.

Hata hivyo,Kamanda huyo pia alihadharisha wazazi wawe makini katika kutunza na kuwalea watoto wao katika kipindi hiki cha sikukuu na kwambae ndapo kutaokotwa mtoto amepotea,mzazi atawajibika kisheria na kupotea kwake mtoto huyo.

“Kiukweli tunatoa angalizo kwa wazazi wawe makini na watoto katika sherehe hizi za Eid elFitri,mtoto akipotea mzazi atawajibika yeye mwenyewe sababu jukumu la kuleana kutunza mtoto ni la mzazi, sasakwaniniumuachehadiapotee,” alisema Kamandahuyo.

Katika hatua nyingine jeshi hilo limetoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuahakikisha wanazingatia sheria za usalama barabarani katika kipindi hiki cha sikukuu ikiwemo kujiepusha na unywaji wa pombe huku wakiendesha vyombo hivyo kwa kuata sheria iliyopo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment