Friday 20 June 2014

HALMASHAURI YA WILAYA YA HANDENI INAPIGANIA KUONGEZA MAPATO YA BIASHARA KUPITA MAZAO.

Diwani wa kata ya  Mkata wilayani Handeni Mussa Mwanyumbu akizungumzia zao la ufuta lilivyo anza kukubalika dhidi ya wakulima wa kata hiyo huku akisisitiza wakulima kulilima kwa wingi ili kuweza kujiongezea kipato.

Mwenyekiti wa kijiji cha  Kwachaga Turiani Miraji Ahamed akielezea namna ya  matumizi ya trekta katika kijiji hicho ambalo walilinunua  kwa lengo la mradi wa kijiji na kuwaongezea kipato ambapo mkulima hukodi trekita hiyo kwa gharama ya shilingi 40,000 kwa ekari moja.

Kaimu  afisa kilimo ,umwagiliaji na ushirika Yibarila  Chiza Kamele akizungumza na baadhi ya waandishi  hawapo pichani kuhusu  masuala mbalimbali ya kilimo cha mazao na upatikanaji wa rutuba ilinayofaa kwa kilimo hivyo wamewataka wakulima kutilia mkazo  kilimo cha kitaalamu ambacho kitafanya kuwaongezea mazao.



Diwani kata ya Ndolwa   wilayani Handeni Joel Mabula ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya huduma za jamii ambazo ni elimu,afya,maji na maendeleo ya jamii  ambapo alielezea   baadhi ya changamoto mbalimbali zinazo  wakabili wananchi ikiwemo masuala ya  uhaba wa vituo vya afya na upatikanaji wa madawa.

No comments:

Post a Comment