Sunday 15 June 2014

MASHINDANO YA POLISI CUP WILAYANI MUHEZA YANAENDELEA KUTIMU VUMBI KATIKA UWANJA WA JITEGEMEE.



TIMU ya soka Contract yenye maskani yake kijiji cha mamboleo wilayani hapa inategemea kushuka dimbani kumenyana na Polisi Jamii ya kambi ya FFU Majani mapana mkoani Tanga.
Mchezo huo wa mwendelezo wa michuano ya Polisi Cup unategemewa kufanyika jumamosi wiki hii katika uwanja wa Jitegemee uliopo wilayani Muheza.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga,Coastantine Massawe amesema kwamba jumla ya timu nne(4)zimefanikiwa kuendelea na hatua hiyo ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Alisema kuwa mashindano hayo yanalengo la kutoa elimu kwa jamii na kuwa karibu na jamii ili kuweza kuwafichua wahalifu kupitia mchezo huo wa soka na kuimarisha ulinzi na usalama mkoani hapo.
“Tangu jeshi la polisi kuanzishwa utaratibu huu kuandaa mashindano ya mpira wa miguu yaliyokuwa yakifahamika kombe la Kamanda Cup,,yamesaidia kuwafichua watu ambao hawana uzalendo na nchi yetu kwa kujihusisha na uhalifu”alisema Massawe.
Mashindano hayo ambayo yamekuwa endelevu kufanyika mkoani hapo kwa makamanda kukabidhiana yalianza mwaka 2009 kwa kushirikisha timu ya polisi na jamii ambayo ni wenyeji.
Massawe alizitaja timu nyingine ambazo zimefanikiwa kuendelea kwenye mashindano hayo kuwa ni Lusanga Fc na Veteran ya wafanyabiashara wilayani Muheza.
Aidha alitumia nafasi hiyo kwa kuvitaka vilabu shiriki kuitumia fursa hiyo kwa kuibua na kuendeleza vipaji vya ili waweze kuonekana na kufika mbali kisoka.

No comments:

Post a Comment