Monday 16 June 2014

WADAU WA ULINZI NA USALAMA MKOANI TANGA WAELEZA CHANGAMOTO MBALIMBALI NA KUTAKA JESHI LA POLISI KUWEKA USHIRIKIANO WA PAMOJA.

Aliyekuwa akichangia hoja katika mkutano wa wadau  wa ulinzi na usalama mkoani Tanga ni OCD  Leonard Nyaoga  kutoka wilayani  Mkinga. 

Mwenyekiti wa mtaa wa mwakizaro  Mabawa Tanga mjini   Sarai Zecha akishauri  mifuko iliyoibuliwa ya wafanyabishara ilenge zaidi kusaidia makundi yaliyoibuliwa  ya ulinzi na usalama kwani baadhi ya vijana wamekuwa wakikamata wahalifu na kuwadhuru bila kuwa na elimu ya ukamataji salama ambapo mfuko huo unaweza kusaidia  kutoa elimu.Add caption

Katibu wa  chama cha bodaboda wilaya ya Tanga aliyesimama akitoa ushauri kuwezeshwa kundi la waendesha  bodaboda   ambao wamekuwa wakiwafahamu wahalifu kwa kuwa ni miongoni mwa  abiria wanaowabeba na kwenda kufanya uhalifu ikiwa zaidi hutumia usafiri  huo na kuachana na magari,hivyo mpaka sasa kuna madreva zaidi ya 600 na waliopatiwa elimu ni 350 pekee.

Askofu mstaafu wa kanisa la  Kombezi   akichangia mada ya ulinzi na usalama ambapo amesema kuwa miongoni mwa mambo wanayoyakemea kwa waumini ni  kuondokana na mambo ya uhalifu ikiwa hata hao wanaofanya uhalifu hukimbilia makanisani.



Kamishina mwandamizi kutoka makao makuu  ya polisi jijini Dar-es-salaam   Faustine Shigole  akiwaeleza wadau walioshiriki   mkutano huo kuhusu jeshi la polisi lilivyo weka mikakati ya uundwaji makundi kutoka ngazi  za  vijiji hadi kata  na kuendesha mashindano  ya polisi cup ili kuweza kupunguza wimbi la uhalifu kwa vijana wanaochipukia kutafuta maisha bora.Add caption

Mkuu wa  usalama barabarani mkoani Tanga akikanusha kuhusu hoja iliyoibuliwa na wadau kuwa baadhi ya askari wa usalama barabarani wamekuwa wakipokea rushwa   hasa kwa kuwakamata  madreva bodaboda ambapo aliwaeleza kuwa wao wasiwe  chanzo ya kumalizana kwa makosa yanayofanyika bali inatakiwa kufuata sheria ndipo rushwa hiyo itaondoka .

No comments:

Post a Comment