Thursday 13 November 2014

Fainal ya michuano ya Malaria Cup wilayani Kilindi ilivyovunja rikodi

 Kikosi kipya cha soka Dogodogo fc wakiwa na viongozi wao siku ya ufunguzi wa mashindano ya Malaria Cup uwanja wa mabombwe wilayani Kilindi kilivyoanza kwa kuomba.
 Mkono wa kushoto ni mgeni rasmi,Kulwa Majibululu aliyemwakilisha mkurugenzi wa halimashauri hiyo ya kilindi akimkabidhi zawadi kapteni wa timu ya Dogodogo Fc mara baada ya kuibuka bingwa wa Malaria Cup Kilindi kwa kuifunga timu ya Town Star kwa magoli 2-0.
 Anayeongea mkono wa kushoto ni mgeni rasmi afisa elimu vifaa na takwimu wilaya ya Kilindi,Kulwasolo Majiyabululu akilishukuru shirika la PSI Tanzania kwa kutoa elimu juu ya ugonjwa wa malaria kupitia mchezo wa soka siku ya fainali akiwa na afisa michezo wa wilaya hiyo Beno Eugene.
 Mashabiki wakiwa na baadhi ya wachezaji wa timu ya Town Star iliyofungwa goli 2-0.mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainal wakisubiri kukabiziwa zawadi za timu shiriki mpira moja kila timu.
Mashabiki wa timu ya mpya ya Dogodogo wilayani Kilindi wakishangiria na kuingia uwanjani mara baada ya kumalizika mchezo wa fainal kabla ya kugaiwa zawadi zao za ushindi za Malaria Cup sherehe zilikuwa hivi.

No comments:

Post a Comment