Saturday, 31 January 2015

Bonanza la michezo la watumishi wa mahakama na wanasheria mkoani 2015 lilikuwa hihi,

Pichani mkono wa kushoto anayeongea ni mgeni rasimi katika bonanza la michezo Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu ya Tanga,Projest Rugazia akiwaeleza wachezaji lengo la kuandaa bonanza hilo kuwa ni moja ya kuikaribisha sherehe za shughuli za mahakama 2015 iliyofanyika viwanja vya Popatlaly jijini Tanga.
Timu ya soka ya wanasheria wa mkoa wa tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya mchezo wao dhidi ya timu ya mahakama ya Tanga.
Kikosi cha mahakama za mkoa wa Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja ambacho kilishuka dimbani.
Baadhi ya wachezaji wa timu ya Netball ya mahakama ya wilaya ya Tanga ambao waliwafunga mahakama kuu ya Tanga kwa magoli 8-1,katika bonanza hilo.
Wachezaji baadhi wa timu ya Netball ya Mahakama kuu ambao wakiwa kwenye picha ya pamoja siku ya bonanza la kuikaribisha siku ya mahakama mkoani Tanga ambao walitoka kwa matokeo ya kichapo cha magoli 8-1,
Mchezaji wa timu ya Mawakili Erick Akaro mara baada ya kupasha kujiandaa na mchezo wa kuwakabili Mahakama ambao ulizaa matunda walitoka kifua mbele kwa kuwafunga wapinzani wao Mahakama kwa goli 1-0.
Pichani ni mchezaji wa timu ya Mahakama Nolel Kiagio akipasha kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Mawakili
Pichani mkono wa kulia ni mgeni rasmi Jaji mfawidhi wa mahakama kuu mkoa wa Tanga,Projest Rugazio siku ya bonanza la michezo akiikagua timu ya Mawakili wa mkoa wa Tanga katika uwanja wa Popatlaly.
  Picha mkono wa kushoto mwanaume ni Jaji mfawidhi wa Mahakama kuu mkoa wa Tanga,Projest Rugazia akiikagua timu ya Netball ya Mahakama kuu Tanga kabla ya kuanza bonanza hilo.

No comments:

Post a Comment