Katikati mwanamke ambaye ameshika ndoo ni mtumishi wa idara ya uhamiaji akigawa chakula kwa waEthiopi 51 mara baada kuwasilishwa ofisi ya mkoa.
WaEthiopia 51 waliotelekezwa pori wilayani korogwe wakiwa ndani ya gari ya idara ya uhamiaji baada ya kusomewa shtaka lao la kuingia nchi bila kibali wakielekea gereza la maweni lililopo jijini Tanga.
Raia wa Ethiopia 51 waliokamatwa wilayani korogwe baada ya kutelekezwa porini wakiwa ofisi ya idara ya uhamiaji mkoa wa tanga wakipata chakula mara baada ya kufikishwa kabla ya mahojiano.
WaEthiopia 51 wakiwa eneo la mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tanga eneo la kuwegesha magari wakiwa na mwendesha mashtaka wa idara ya uhamiaji Hamisi Juma ambaye amesimama kavaa suti nyeusi wakisubiri kuingia mahakamani kusomewa kosa lao la kuingia nchi bila kibali.
WaEthiopia wakiwa mahakama ya hakimu mkazi wakisubiri kusomewa shtaka linalo wakabili.
No comments:
Post a Comment