Kapteni timu ya Qeen Tanga,Tedy Simba amesema wanatarajia kuondoka na kikosi cha watu 25 wakiwemo wachezaji na viongozi,pia ameongeza kwamba kutokana na maandalizi wanayoyafanya huenda ikawa tishio katika mashindano hayo kutokana na wachezaji mahili wenye vipaji wanaotegemea kuondoka nayo kuunga msafara huo.
Kocha wa kikosi cha timu ya Qeen Tanga,Debora Mzava akizungumzia jinsi maandalizi ya kujiandaa na mashindano ya netball yanayo tarajiwa kufanyika mkoani Mwanza mwaka 2015.ameomba wadau wajitokeze kuwasapoti na watahakikisha wanauwakilisha mkoa na kurudi na ushindi.
Kapteni wa timu hiyo amesema wako mbioni kusaka million 17,ili kuwawezesha kwenda kushiriki mashindano hayo.
Wachezaji wa kikosi cha Tanga Qeen huku wakisaka fedha kwa wadau za kwenda kushiriki wakijinoa katika uwanja wa polisi Chumbageni uliopo jijini Tanga.
No comments:
Post a Comment