Pichani ni mchezaji chipukizi ambaye amenufaika na shirika lisilo la kiserikal CHRISC akizungumzia jinsi alivyoweza kuibua na kuendeleza kipaji chake,Mkuu Ally.
Mkuu juzi akizungumza na mkurugenzi wa Wakati Sports Blog juu ya maandalizi yake katika kuitumikia nafasi ya kipa tangu akiwa na umri mdogo na kufanikiwa kuchezea timu mbalimbali mkoani tanga.
Amesema amelelewa na shirika la CHRISC baadae aliweza kutumikia timu za Vasco Dagama,Middo Veterani na Coastal Union B. malengo yake anataka kufuata nyayo za mchezaji Aishi Manula mlinda mlango wa timu ya Azam ya jijini Dar es alaam.
Pichani ni katibu wa shirika la CHRISC mkoani Tanga, Hatibu Shabani mara baada ya kutoa semina ya siku tatu juu ya masomo matatu Hisabati,Sayansi na Kiingereza akizungumzia lengo la kuandaa semina hiyo.
Hatibu amesema ni kuwaandaa wanafunzi wa darasa la sita nala saba kuweza kufanya vizuri katika mitihani yao ikiwemo kufaulu.
Pichani kati kati ambaye amevaa fulana nyeupe ni miongoni mwa walimu katika semina hiyo,Victar Stanslaus akitoa mafunzo kwa vitendo juzi katika shule ya msingi Kwakaeza semina iliyoshirikisha shule mbili Donge na Kwakaeza jijini Tanga.
Pichani Katibu wa CHRISC Tanga,Hatibu akifafanua mikakati yao katika kuibua na kuendeleza vipaji mbalimbali mkoani hapo.
Pichani ni miongoni mwa wanafunzi,Sakina Nassoro mara baada ya semina hiyo akizungumzia faida na changamoto ya masomo hayo amesema ni magumu na walimu hawatoshi.
Sakina amesema kutokana na changamoto hizo inapelekea baadhi yao kusitisha masomo na kuchangia utoro katika shule mbalimali za msingi.
Mwanafunzi,Sakina ameishauri serikal kutoa kipaumbele kwa kuajili walimu wengi wenye taaluma ya masomo hayo ili waweze kunufaika nayo.
Pichani ni baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye makundi kujinoa na masomo hayo.
Pichani ni mtoto mwenye miaka miwili,Magreti Victar ambaye anauwezo mkubwa wa kuhesabu mpaka mia sita akiwa kwenye shule ya msingi Kwakaeza akifuatilia masomo hayo.
Mtoto huyo ameonekana kutokea kuipenda elimu akiwa na umri mdogo na kupenda kujichanganya na wanafunzi wa shule ya msingi,
Pichani ni mtoto,Magreti akiwa na baba yake Victar Stanslaus ambaye ni mwalimu shule ya msingi Kwakaeza.
No comments:
Post a Comment