Wednesday 15 February 2017

UZINDUZI WA DARAJA KIJIJI CHA VETA LINALOUNGANISHA LUSHOTO NA BUMBULI ILIKUWA HIVI,,

 Picha mkoni wa kulia ambaye amevaa suti ya kijani ni mwenyekiti wa halmashauri ya Lushoto,Lucas Shemndolwa akifuatiwa na mkuu wa wilaya hiyo January Rugangika na katibu mwenezi wa CCM wilayani hapo Mzee Kirua wakifungua daraja la Zeti ili kuwaondolea usumbufu wanafunzi ambapo kipindi cha mvua walikuwa wanashindwa kwenda shule.
 Mara baada ya kukata utepe wa ufunguzi wa daraja hilo,Shemndolwa viongozi wakifurahia,,
 Mwenyekiti wa halmashauri ya Lushoto ambaye ni mgeni rasmi,Shemndolwa mara baada ya kufungua akisoma maandishi.
 Mwenyekiti akisoma maandishi ambayo yameandikwa.
 Viongozi wakisubiri utaratibu.


 Mkono wa kushoto ni mkuu wa wilaya hiyo ya Lushoto,akiwa na diwani wa kata ya Hubiri,Omari Ramadhani ambaye amevaa suti nyeusi na wananchi mara baada ya kufunguliwa wakipita.
 Katikati ni diwani wa kata hiyo akisalimiana na wananchi wake na kata jirani ya Vuga halmashauri ya Bumbuli.
 Mkurugenzi wa halmashauri ya Lushoto,Makwega Kazimbaya ambaye amesema katika kufanikisha ujenzi huo wametumia sh.8,800,000/= za kitanzania ambapo awali walikuta taarifa ukihitaji million 100,
 Diwani wa kata jirani ya Vuga,Dhahabu akizungumza juu ya mafanikio yatakayopatikana kukamilika kwa daraja hilo mbali na kuondoa changamoto kubwa ya watoto kipindi cha mvua.

Pichani ni miongoni mwa watoto 150 ambao kipindi cha mvua walikuwa wanashindwa kwenda shule kutokana na daraja la Zeta kujaa maji wakiwasikiliza viongozi na mwalimu wao katika hafla hiyo ya ufunguzi huo wa daraja.

No comments:

Post a Comment