Monday 22 May 2017

KAMANDA WA POLISI TANGA,WAKULYAMBA AKIONYESHA SILAHA 4 ZILIZOTUMIKA KWENYE MATUKIO YA UJAMBAZI LIKIWEMO LILE LA MAUAJI WILAYANI KILINDI,

 Pichani kati kati ambaye amevaa sare ya polisi ni kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba na kushoto ni Ofisa upelelezi wa mkoa huo,Amedeu Tesha na kulia ni mlinzi maalum askari kitengo cha FFU,Gasper leo ofisini kwake akiwaonyesha waandishi wa habari ambao (hawapo pichani) silaha nne za kutengeneza ikiwemo Shortgun zilizotumika kwenye matukio tofauti ya ujambazi likiwemo lile la kuvamia nyumba wilayani Kilindi na kumuua Mohamed Ally.

Pichani kati kati ambaye amevaa sare ya polisi ni kamanda wa polisi mkoa wa Tanga,Benedict Wakulyamba na kushoto ni Ofisa upelelezi wa mkoa huo,Amedeu Tesha na kulia ni mlinzi maalum askari kitengo cha FFU,Gasper jana ofisini kwake akiwaonyesha waandishi wa habari ambao (hawapo pichani) silaha zote nne 4 za kutengeneza ambazo zinasadikiwa kutumika katika matukio mbalimbali ya kijambazi likiwemo la tukio la kuvamia nyumba wakiwa na silaha,mapanga na kumuua Mohamed Ally huko wilayani Kilindi.

 

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI la Polisi mkoani Tanga linawashikilia watu wanne akiwemo Yohana Sendeu (41)mkazi wa Kibaigwa mkoani Dodoma na Elisha Isaya (24) mkazi wa Gairo Morogoro wanaosadikiwa kuwa majambazi baada ya kupatikana na Silaha mbili moja aina ya Shortgun na nyingine Pistor ambazo zimetengenezwa kienyeji zinasadikiwa kuwa zilitumika kwa matukio ya uhalifu.


Hata hivyo imeelezwa kukamatwa kwa watuhumiwa hao ni baada ya tukio la lililotokea kitongoji cha Msaneni huko kijiji cha Kwekivu wilayani Kilindi ambapo Mohamedi Ally alivamiwa nyumbani kwake na majambazi hayo na kufanikiwa kumpiga risasi kwa kutumia silaha aina ya Gobore kwenye ubavu wa upande wa kushoto hadi kumuua.


Kamanda wa Polisi mkoani Tanga,Benedict Wakulyamba amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema watuhumiwa hao walikamatwa huko katika kijiji cha Msaneni,Kwekivu wilayani Kilindi ambapo Yohana Sendeu ni mkazi wa Dodoma na Elisha Isaya mkazi wa Gairo Morogoro wote wanaendelea kushikiliwa.


Kamanda Wakulyamba alisema katika mahojiano na polisi watuhumiwa hao walionyesha silaha mbili moja ikiwa gobore na nyingine Pistor ambazo zote zilitengenezwa kienyeji zikitumia risasi za Shotgun ambapo zilikuwa zimefichwa porini baada ya kutumika kwenye tukio la mauaji lililokuwa limefanyika.


Alisema kwamba katika mahojiano hayo na watuhumiwa hao pia yaliwezesha kupatikana watu wengine wawili ambao ni Omari Selemani maarufu ‘Chang'oma Dipochi’ (39) mkazi wa Chamtui Handeni na Salum Selemani maarufu Chang'endo (54) ambaye ni mkazi wa Chamtui kwenye wilaya hiyo ya Handeni mkoani Tanga.


Aidha,ameitaja Silaha aina ya Shotgun ambayo imekamatwa kuwa ni ile yenye nambari MG 873 A ambapo watuhumiwa wanaodaiwa kuhusika kwenye matukio ya mauaji huko Tanga na Dodoma wote wanne wakiwa wanaendelea kushikiliwa na polisi uchunguzi huku ukiwa unaendelea.


“Watuhumiwa wote wanaendelea kushikiliwa polisi kwa mahojiano na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani ili kuweza kujibu mashataka yatakayokuwa yakiwakabili”alisema kamanda huyo wa Polisi mkoani Tanga huku akiwasihi raia wema kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi.


Katika tukio jingine kamanda Wakulyamba alisema kuwa huko kwenye mtaa wa Mtakuja kijiji cha Mkalamo tarafa ya Mkwaja wilayani Pangani amekamatwa Yusuph Ally (19) mkazi wa Handeni akiwa na silaha aina ya Pistor iliyotengenezwa kienyeji ikiwa na risasi nne na mtuhumiwa anachunguzwa.


Alisema kuwa katika tukio hilo mara baada ya uchunguzi wa polisi kukamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa taratibu za sheria kuchukua mkondo wake ambapo pia kamanda huyo wa polisi mkoani Tanga alitumia fursa hiyo kuzungumza na wanahabari kutahadharisha usalama wa barabarani.


Wakulyamba alisema ingawa barabara ya kutoka Mombo kwenda Lushoto iliyokuywa imezuiliwa kutumika kwa sasa imefunguliwa lakini iko haja kwa wasafirishaji kuchukua tahadhari ya usalama kutokana na ukweli kwamba bado tathimini na hatua za kufanya ukarabati unaendelea kufanyika.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment