Sunday 11 June 2017

MAONYESHO YA TANO YA BIASHARA 2017 MKOANI TANGA YALIKUWA HIVI,,,

 Pichani mkono wa kulia mwanamke ni katibu tawala wa mkoa wa Tanga,Zena Said ziara yake akitembelea mabanda la halmashauri ya Handeni maonyesho ya tano ya biashara mwahako mkoani hapo,

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
SERIKAL mkoani Tanga imezitaka kada za vijana na wakina mama kuelewa kwamba mikopo wanayopatiwa siyo zawadi na wanapaswa kurejesha baada ya kuitumia katika kutekeleza miradi yao ya uzalishaji mali huku lengo likiwa kuweza kujikwamua kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa juzi na katibu tawala mkoa wa Tanga,Zena Said wakati alipotembelea mabanda ya maonyesho ya biashara huko eneo la Mwahako Jijini Tanga huku akielezea kutoridhishwa kwake na ushiriki mdogo wa kada ya vijana katika shughuli hiyo ambayo ingekuwa fursa kwao kujikwamua.

Alisema kuwa serikali yao imekuwa ikitoa fedha kupitia kila halmashauri ambapo kuna asilimia zilizotengwa maalum kwa ajili ya makundi hayo ili kuweza kutumika kwa kuendesha shughuli mbalimbali za uzalishaji mali akiwataka kuitumia vyema fursa hiyo katika kuanzisha miradi ya kimaendeleo.

Katibu tawala huyo,Zena alisema kwamba fedha hizo ambazo ni mikopo sio kama zinatolewa kama zawadi na zimelenga kuwasaidia kuendesha shughuli za kiuchumi huku akisema wale watakaobahatika kupewa fedha hizo wanapaswa kuzitumia kuendesha miradi na kurejesha hatua ambayo itasaidia wenzao kukopeshwa.

“Kiu kweli zipo  asilimia mnazopaswa kukopeshwa sio kwamba zinatolewa tu bali ni mkopo unaotolewa kwa utaratibu ili uwasaidie kuendesha shughuli zenu “serikali imedhamiria kuwasaidia vijana hivyo ni juu yenu kujitokeza kwa kufuata masharti ya kujiunga vikundi na kuweza kuzitumia hizo fursa “alisema Zena.

Aidha,alibainisha kwamba lengo kubwa la serikali ni kuwawezesha vijana kupata mitaji kuendesha biashara zao huku akiwasihi wakazi wa Jiji la Tanga kujitokeza kwa wingi ili kuweza kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na mashirika na taasisi za umma na pia wajasiriamali kupata kufaidika na fursa zilizopo.

Katibu tawala huyo ametumia nafasi hiyo kutoa angalizo kwa vijana na wanawake wasio na fedha kujitokeza ili kukopeshwa na kuondokana na dhana ya kuona kile wanachopatiwa kuwa ni sawa na zawadi bali imelenga kuwaendeleza mitaji yao akiwataka kufuata taratibu stahiki za masuala ya mikopo.

 Naye,Mtani Manundu ambaye ni afisa mshauri wa biashara wa Benki ya CRDB jijini Tanga amesema kwamba wamekuwa wakiyatumia maonyesho hayo katika kuielimisha jamii namna ambavyo wanaweza kunufaika na mikopo kutoka kwenye asasi za fedha ikiwemo benki yao kwenye matawi mbalimbali.

Vile vile Augustino Kasale ambaye ni Afisa uhusiano wa serikali alisema shirika la maendeleo ya Petrol Tanzania TPDC wanatumia maonyesho hayo kuelimisha jamii kuona fursa ikiwemo ile ya gesi kupitia mradi mkubwa wa bomba la mafuta akiamini kwamba wananchi walio wengi watanufaika.
Mwisho.



No comments:

Post a Comment