Monday 8 May 2017

MAOMBI YA KUWAOMBEA WANAFUNZI KUHUSU AJALI YA VIFO ARUSHA,MKOANI TANGA ILIKUWA HIVI,

 Mchungaji wa kanisa la Sabato kana jijini Tanga na mratibu,Jackson Gladson Mding"u katika kuomboleza kimkoa ajali iliyouwa wanafunzi,walimu na mzazi kwa mshtuko mkoani Arusha akisoma taarifa yake kwa kwamba imegusa watu wengi ikiwemo shule yake ya Kana Central English Medium Primary na Nursery school kwani walishaanza urafiki na shule hiyo.
 Pia, mchungaji wa kanisa hilo la Sabato kana jijini hapo,Jackson Mding’u alisisitiza kusema kuwa wanafunzi hao walitarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa Taifa hili ambapo aliwasihi watanzania kuendelea kuungana kudumisha upendo.

" Kanisa la sabato tutaendelea kumuunga mkono rais Dk.John Magufuli na kuonyesha uzalendo kwa wilaya na Taifa letu"
 Pichani ni shehe wa Baraza la waislam (BAKWATA),Mohamed Mbaraka akieleza kusikitishwa kwake  na baadhi ya mitandao ya kijamii kueleza katika ajali hiyo alinusurika Muislamu mmoja tu ambapo ameiomba serikali kuangalia namna ya kuwashughulikia watu wa namna hiyo kwa sheria ya mitandao wanaoeneza lugha ambazo zinachangia kupotosha jamii ya kitanzania akashughulikiwa kwa mujibu wa sheria iliyopo ili kulinda amani iliyojengeka.
 Pichani ni mchungaji Msumari akieleza jinsi masikitiko yake kutokea kwa ajali hiyo.
 Pichani ni kaimu afisa elimu wa jiji la Tanga,Rose Ngowi akiwashauri walimu wa shule hiyo iliyokubwa na tatizo hilo,kipindi hiki kupeleka wainjiristi ili kuwatia moyo wanafunzi katika masomo yao.
 Pichani ni mkuu wa wilaya ya Tanga,Tobias Mwilapwa akiungana na wanafunzi,walimu madhehebu ya dini kuomboleza.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KANISA la Wadventist Sabato Kana Central Jijini Tanga limewaunganisha wanafunzi wa shule ya msingi Chuma,Indian Ocean na Kana Central English Medium kufanya maombi kuhusiana na vifo vya vijana wenzao wa Jijini Arusha,pia wameishauri Serikali kusimamia kwa makini vyombo vinavyotumika kusafirisha Wanafunzi.


Akisoma risala yao waliyoitoa kwenye maombi hayo jana iliyosomwa na Braitiness Chaula wanafunzi hao walisema kwamba,wameshindwa kuvumilia kwa kukaa kimya bila ya kusema lolote ambapo licha ya kupata fursa ya kufanya maombi pia wameamua kutumia nafasi hiyo kuishauri serikali mambo kadhaa ya msingi.


Miongoni mambo walioishauri serikali yao,wanafunzi hao walisema kuwa ingawa hawana weledi wa vyombo vya usafiri lakini wanadhani ni vyema kwa serikali kuvifanyia uhakiki vyombo vya usafiri kuvibaini kama viko salama kwa ajili ya kusafirisha abiria na wanafunzi hasa wale waliopo shule binafsi.


Aidha,wanafunzi hao walisema kwamba vyombo vya usafiri ambavyo havijakaguliwa visiruhusiwe kufanya kazi huku wakitaka wanafunzi na magari husika kukatiwa Bima kabla ya kuanza safari zao hatua ambayo itasaidia kuimarisha usalama kwa watumiaji wa magari husika kwenye shule mbalimbali.


Mchungaji wa Kanisa la Sabato Kana jijini Tanga na mratibu,Jackson Gladson Mding’u alisema lengo la kukutana kwa taasisi hizo za dini ni kuiunga mkono Serikali katika kuomboleza vifo vya wanafunzi na watu wengine waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo iliyotokea Jijini Arusha na kuishtua jamii.


Alisema,ni muhimu kwa wanafunzi kufanya ziara wawapo shule lakini kuna haja ya vyombo vya usafiri kuangaliwa ubora wake kabla ya kuanza kazi huku madereva wanaowasafirisha wanafunzi hao wakiwa wale wenye ubora unaokubalika jambo ambalo litasaidia kuondoa uwezekano wa ajali kujitokeza.


Aidha mchungaji huyo alisema kwamba kumejengeka mazoea kwa baadhi ya matrafiki kutokagua magari ya wanafunzi na badala yake kuyaacha jambo ambalo linaweza kusababisha ajali kujitokeza ambapo amelishauri jeshsi la polisi kukagua kikamilifu magari ya abiria ili kuepuka madhara.


Naye Shekhe Mohamed Mbaraka wa Baraza la waislam (BAKWATA) ameelezea kusikitishwa kwake  na baadhi ya mitandao ya kijamii kueleeza kuwa katika ajali hiyo aliyenusurika ni Muislamu mmoja tu ambapo ameiomba serikali kuangalia namna ya kuwashughulikia watu wa namna hiyo kwa sheria ya mitandao.


Alisema mungu ni mmoja na hachagui ni vyema wanaoeneza lugha ambazo zinachangia kupotosha jamii ya kitanzania akashughulikiwa kwa mujibu wa sheria iliyopo ili kulinda amani iliyojengeka.

Huku mchungaji wa kanisa la Sabato kana jijini hapo,Jackson Mding’u akisistiza kusema kuwa ajali hiyo imegusa watu wengi ambao walitarajiwa kuwa msaada mkubwa kwa Taifa hili ambapo aliwasihi watanzania kuendelea kuungana kudumisha upendo.

Kwa upande wake kaimu afisa elimu wa jiji la Tanga,Rose Ngowi amewataka walimu wa shule hiyo iliyokubwa na tatizo hilo,kipindi hiki kupeleka wainjiristi ili kuwatia moyo wanafunzi katika masomo yao.


Naye mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa alisema,serikali itaendelea kuwa karibu na wananchi wake  na itafuatiulia kwa makini ushauri uliotolewa huku akitumia fursa hiyo kuliagiza jeshi la polisi kufanya ukaguzi kwa madereva ambao wanajihusiaha na vitendo vinavyosababisha ajali kama ulevi.


Vilevile mkuu huyo wa wilaya ya Tanga alisema kwamba mkakati madhubuti utawekwa kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva wazembe watakaopita kwenye alama za vivuko bila ya kuchukua tahadhari ya kusimama akitanabaisha kuwa moja ya adhabu watakazopewa ni leseni kufungiwa.

Hata hivyo maombezi hayo yaliyofanyika shule ya
Kana Central English Medium kwa kuwaunganisha wanafunzi wa shule na madhehebu ya dini mbalimbali moani hapo.
Mwisho.
 Viongozi wakiomba.



 Wanafunzi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Tanga,juu ya madereva ambao watavunja sshria kwenye vivuko.,
 Wanafunzi wakiimba mwimbo wa kuiombea Tanzania na rais Dk.John Magufuli.
 Wanafunzi.
Pichani ni baadhi ya wanafunzi wakiwasikiliza viongozi wa dini mbalimbali.

No comments:

Post a Comment