Sunday 7 May 2017

ZIARA ZA JUMA LA ELIMU KIMKOA WILAYANI KOROGWE ILIKUWA HIVI,,

 Picha mkono wa kushoto ambaye amevaa suti nyeusi ni mkuu wa mkoa wa tanga,Martine Shigella siku ya juma la elimu akiwasili kwenye shule ya sekondari Mnyuzi iliyoko wilaya ya Korogwe vijijini akiwasalimia viongozi kutoka halmashauri mbalimbali mkoani hapo kabla ya kutembelea miradi ya sekta ya elimu.
 Katika ni mkuu wa mkoa wa tanga,Shigella mkono wa kushoto ni msaidizi waki na kulia ni mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robart Gabriel akimuongoza kukagua majengo mapya vyumba vya madarasa na mabweni mawili.
 Mkuu wa mkoa wa Tanga,Shigella akisalimiana na katibu mpya wa chama cha mapinduzi wa Korogwe mji,
Pichani ni mkuu wa mkoa wa Tanga,Shigella mara baada ya kukagua majengo ya shule sekondari Mnyuzi akiwahutubia wananchi na wanafunzi na mvua .

NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE

MKUU wa mkoa wa Tanga,Martine Shigella amewataka wananchi wa kata ya Mnyuzi kuwapokea vizuri watumishi wanaofika kwenye maeneo yao lengo likiwa kuwawezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na tija ambapo pia alitumia fursa hiyo kuwataka kusaidia kuimarisha ulinzi kwenye shule zao.


Shigella aliyasema hayo juzi alipotembelea kijiji cha Mnyuzi mahali ambapo kumeendeshwa mradi mkubwa wa ujenzi wa vyumba vya madarasa na mabweni mawili ambapo alieleza kuridhishwa kwake juu ya kazi zilivyofanyika huku akiwataka wadau wengine kuiga mfano kwenye ujenzi huo uliofanyika wilayani hapo.


Katika ziara yake hiyo alikuwa ameambatana na wakuu wa wilaya zote za mkoa wa Tanga,wakurugenzi watendaji,maafisa elimu na hata wenyeviti wa halmashauri na wale wa chama cha mapinduzi CCM ambapo kwa umoja wao walisema wameridhishwa na kazi jinsi ilivyotekelezwa.


Akizungumza mara baada ya kumaliza kukagua majengo ya shuleni hapo,Shigella alisema kwamba wananchi wanapaswa kusaidia kuimarisha ulinzi kwenye miundombinu hiyo huku akiwasihi kuwapokea kwa ukaribu watumishi ambao wamekuwa wakipangiwa kufanya kazi kwenye maeneo ya vijiji vyao.


Aidha mkuu huyo wa mkoa aliwapongeza wakazi wa kata ya Mnyuzi kwa mchango wao mkubwa waliouonyesha kwenye ujenzi wa miundombinu ya shule hiyo akisema ameridhishwa na taarifa za ushiriki wao kwenye ujenzi huo akiwaomba wananchi hao kuendelee kushirikiana na Serikali yao.


“Watumishi wakija tuwapokee vizuri kufanya hivi itatusaidia katika kuwawezesha kufanya kazi kwa tija,vilevile tusaidiane kuimarisha ulinzi kwenye majengo yetu haya”alisema mkuu huyo wa mkoa wa Tanga ambaye alitembelea miradi mbalimbali ya elimu upande wa halmashauri za Korogwe mji na Korogwe vijijini.


Kwa upande mwingine mkuu huyo wa mkoa wa Tanga aliwataka wananchi hao wa kata ya Mnyuzi kuangalia uwezekano wa kuzuia mifugo isipite kwenye eneo ambalo ni katikati ya shule hiyo akiwataka kuanzisha mchakato wa upatikanaji njia nyingine kwa ajili ya kuimarisha usalama na uhifadhi mazingira.


Wakati huo huo mkuu huyo wa mkoa wa Tanga aliwataka wananchi kushiriki kilimo cha zao la mihogo hatua ambayo itawawezesha kuepukana na uwezekano wa kukumbwa na upungufu wa chakula huku akiasa tabia za baadhi ya watu kujihusisha na uuzaji wa mahindi mabichi jambo ambalo huleta njaa.


“Marufuku watu kuuza mahindi mabichi hii itatuleta shida ya chakula,pia inakuwa vigumu kujua ni nani amechukua mahindi ya mwenzake bila kuruhusiwa,nitumie fursa hii kuwaagiza ma DC wote kusimamia kutokusafirishwa kwa mahindi mabichi hii itatuletea shida”alisema RC Shigela.


Mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella alikuwa wilayani Korogwe ambapo alitembelea miradi ya ujenzi shule ya msingi Kilimani,Gereza na shule ya sekondari Mnyuzi ambapo alijionea ubora wa miradi hiyo.

Mwisho.
 Pichani ni viongozi kutoka halmashauri zote za mkoa wa Tanga,wakiwemo walimu juzi wakiwa kwenye ukumbi wa halmashauri ya Korogwe vijijin wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tanga (ambaye hayuko pichani)

NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
MKUU wa mkoa wa Tanga,Martine Shigela amewataka Walimu kuhakikisha kuwa Juma la elimu linakuwa chachu ya kuboresha shule na maabara hatua itakayosaidia upatikanaji wa wataalama wa kutosheleza na hivyo kuwa na Taifa la watu wenye weledi na kuharakisha maendeleo.

Shigella aliyasema hayo juzi alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa wadau wa elimu katika mkutano wa Juma la elimu ambao ulifanyika wilayani Korogwe akisema,lengo la kufanya hivyo ni kujipanga juu ya elimu kwa kusomesha watoto na kukabiliana na tatizo la Mimba kwa wanafunzi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa wa Tanga alizungumzia changamoto ya Mimba akisema kwamba bado kuna tatizo kubwa la Mimba kwa wanafunzi kwenye shule zilizopo ambapo wazazi na walezi wameonekana kutotilia umakini katika kufuatilia juu ya suala hilo akihimiza uundwaji wa sheria ndogo kudhibiti.

Vilevile Shigella katika kikao hicho cha elimu amezitaka Halmashauri kuwatumia mafundi wa ndani katika kufanikisha  ujenzi wa miradi ya sekta ya elimu ili kuweza kupiga hatua za haraka kwenye maendeleo ya sekta ya elimu agizo ambalo alilitoa mara baada ya kutembelea miradi kabla ya kikao hicho kufanyika.

Kwa upande wake afisa elimu wa mkoa wa Tanga,Mayasa Hashim amekiri hali ya ujauzito kuwa ni mbaya huku akitanabaisha kwamba kwa mwaka 2016 kulikuwa na jumla ya wanafunzi 40 wa darasa la saba walikatiza masomo kwa ajili ya kuwa wajawazito ambapo alikemea vikali tabia hiyo kwa watoto.

Afisa elimu huyo wa mkoa wa Tanga alizitaza baadhi ya wilaya
zilizoathirika kuwa Halmashauri ya Handeni vijijini ilikuwa na
wajawazito 12,Pangani 10,Kilindi 9,Korogwe 7 akiwemo mwanafunzi wa darasa la nne kutoka Halmashauri ya jijini la Tanga.

 Kwa upande wa sekondari  ambazo zilikumbwa na sakata la wanafunzi wake kuwa wajawazito Halmashauri  zilizoongoza ni Kilindi 32,Muheza 25 na Handeni vijijini 25 huku walimu waliokumbwa na vyeti feki ni 9 kwa mkoa wa Tanga na kwamba jitihada zinaendelea kumaliza tatizo.

Naye mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Rboert Gabriel wakati
akichangia mada ya Mimba kwa wanafunzi alisema kwamba imeanzishwa kampeni kabambe kuwabana wale wenye tabia chafu za kuwapa mimba watoto wa shule akisema sheria zinatumika katika kuwashughulikiwa watu hao.

Vile vile,Mhandisi Gabriel alisema kwamba suala la utoro kwa wanafunzi limefanikiwa kudibitiwa wilayani Korogwe ambapo idadi kubwa ya wanafunzi waliopkuwa hawahudhurii masomo wamerejea shuleni huku akisistiza kwamba sheria za elimu zinatumika katika kupinga vitendo hivyo viovu.

Amesema,hatua za kuwalinda wanafunzi zimeanza kuchukuliwa kwa vileimebainika kuwa wafanyakazi wakipata matatizo wanavyo vyama vyao vyakuwasemea tofauti na wanafunzi ambao hawana wa kuwasemea ndio ikaonekana ni vyema jamii hiyo kusaidiwa na dawati la jinsia linalosaidia kutatua kesi.
Mwisho
.

 Pichani ni baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari Mnyuzi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tanga.
 Pichani ni baadhi ya wanafunzi na wananchi wakimsikiliza mkuu wa mkoa wa Tanga siku ya juma la elimu.
Picha ni afisa elimu mkoa wa Tanga,Mayasa Hashim akiwasilisha taarifa ya wanafunzi waliopata mimba za utoto na kukatiza masomo kwa mwaka 2016.

Pia kamezitaja wilaya zinazoongoza kwa kuathirika na tatizo hilo la mimba kwa upande wa shule za msingi ni 40,Handeni,Korogwe,Pangani na Muheza na kwa upande wa sekonda ni Kilindi 32,Handeni vijijini 25 na Muheza 25.

No comments:

Post a Comment