Sunday 1 October 2017

MWENGE WA UHURU 2017 MKOANI TANGA ULIKUWA HIVI,,,





Mkuu wa wilaya ya korogwe,Mhandisi Robart Gabriel mkono wa kushoto akimkabizi mwenge wa Uhuru mkurugenzi mtendaji wa handeni vijiji,Willam Makufwe.

Pichani ni miongoni mwa askari wa jeshi la polisi kitengo cha FFU mkoani hapa wakimbiza mwenge kimkoa
Pichani ni mkuu wa wilaya ya koroge,Mhandsi Robart eneo la mkesha uwanja wa shule ya msingi Mazoezi wilayani korogwe akiwahutubia wananchi. 
Pichani ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Amour Hamad Amour mara baada ya kufungua ujenzi wa zahanati akipanda mti aina ya mfenesi kama kumbukumbu.
Pichani katikati ambaye ameshika kipaza sauti,ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Amour Hamad Amour mara baada ya kusomewa taarifa ya mradi wa shamba la miti aina ya mitiki akiompongeza uongozi kwa mradi huo.
Pichani ni shamba la miti ambalo limemwagiwa pongezi na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru ambapo ameshauri kutumika kwa ajili ya manufaa ya ndani ya nchi badala ya kuuza nje.
Pichani ambaye ameshika kipaza sauti ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Amour akiwasilisha ujumbe wa mwenge na malengo yake.

NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
VYUMBA vya madarasa vyenye kuzingatia ubora wa viwango na gharama za ujenzi kuwa ndogo vimegusa moyo ya wakimbiza Mwenge wa Uhuru ambapo kiongozi wa mbio hizo kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour amepongeza utendaji wa mkuu wa wilaya hiyo.

Amesema,tangu Mwenge kuingia Korogwe na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa wamebaini kutokuwepo harufu ya rushwa na kwamba miradi iliyopo ni ambayo Rais Dk Magufuli anaihitaji kufikia uchumi wa viwanda.

Kiongozi huyo wa Mwenge mwaka 2017 kitaifa Amour Hamad alisema Korogwe imeonyesha umakini katika utekelezaji miradi huku akimpongeza mkuu wa wilaya ya hiyo mhandisi Robert Gabriel kwa kusimamia miradi yenye ubora wa viwango na gharamna zikiwa ndogo.

Hayo yamejitokeza wakati Mwenge wa Uhuru ulipokuwa wilayani humo,akisema tangu walipoanza kuzungukia miradi wamekuwa wakifanya ukaguzi wa kina lengo likiwa kubaini mapungufu na hata hivyo hawakuweza kuyapata kama ilivyokuwa kwa maeneo mengine.

Amour alisema,yeye na wakimbiza Mwenge wenzake wameridhishwa na jinsi kazi zilivyofanyika Korogwe akisema ameshangazwa kuona chumba cha darasa kikiwa kimekamilika kwa kiasi cha shilingi milioni saba na ujenzi kuwa madhubuti kwa viwango.

Kutokana na yale aliyoyakuta wilayani Korogwe,kiongozi huyo wa Mwenge alisema hatasita kufikisha salamu kwa Rais kwa jinsi DC Korogwe (Mhandisi Gabriel) alivyo mchapakazi kwa kuisaidia serikali akiwatumikia wananchi kwa uadilifu na tija ya hali ya juu.

Kiongozi huyo wa Mwenge alimsihi mkuu huyo wa wilaya ya Korogwe kuendelea kushirikiana vyema na watendaji wake sambamba na wananchi huku akimmwagia sifa mbunge wa Korogwe mjini Marry Pius Chatanda kwa kujitolea kusaidia wananchi wake.

Alisema,Chatanda ni miongoni mwa wabunge wachache waliokubali kushirikiana na wananchi kwa karibu ili kutatua kero zilizopo kwenye maeneo yao ambapo alitanabaisha kwamba kuna maeneo wapo wabunge ambao wanakataza wananchi kuchangia maendeleo.

Aidha kiongozi huyo wa Mwenge kitaifa amewataka wananchi kuendelea kumuombea kwa Mungu Rais Dk Magufuli ili kumwezesha kuwatumikia kwa kuleta maendeleo ya haraka huku akibainisha kuwa mkuu huyo wa nchi kila uchao amekuwa mtetezi wa wanyonge.

Pia kiongozi huyo wa Mwenge alitumia fursa hiyo kumpongeza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Korogwe Jumanne Shauri kwa utendaji kazi wake akimtaka kuendelea kushirikiana vyema na viongozi wenzake kutimiza azma ya serikali ya awamu ya tano.

Alimtaka kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha kwamba fedha za wanawake na vijana zinaleta tija kwa jamii husika ambapo mkurugenzi alimjibu kuwa wamejidhatiti kwa hilo.

Akizungumzia jinsi walivyojipanga katika kuyainua makundi hayo maalum,mkurugenzi huyo wa Mji,Jumanne Shauri alisema,wamejiupanga kuwatengea eneo maalum vijana na wanawake huku wakiwaanzishia shughuli ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Mwisho.

NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
KIONGOZI wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour amesisitiza umuhimu wa Halmashauri kufungua milango kwa wawekezaji akitaka mwekezaji,Allexander Masoni kuendelea kuwekeza kwenye sekta ya viwanda vidogo hatua itakayoweza kuongeza fursa ya ajira kwa wananchi.

Amour aliyasema hayo leo baada ya kuonyesha kuridhishwa na mfanyabiashara huyo anayemiliki Hotel ya Buggati kuimarisha mfumo wa ulipaji mapato ya Serikali akitumia mashine za Kielektroniki EFD ikiwa ni hatua mojawapo ya kuungana na Rais Dk.John Magufuli akiwataka wananchi kulipa kodi kwa maslahi ya Taifa lao.

Kuhusu ujenzi huo ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2009 na kukamilika mwaka 2914 kwa  kutumia sh 400 milioni ingawaje umeweza kutekelezwa katika vipindi mbalimbali kulingana na upatikanaji wa rasilimali fedha yote hayo yakiwa yalibainishwa kwenye taarifa iliyowasilishwa na Khalid Nyoni.

Baada ya taarifa ya mradi huo kusomwa na mwakilishi wa mwekezaji kwa kiongopzi wa mbio za Mwenge kitaifa,Amour Hamad Amour alisema mbali na uwekezaji huo kutoa huduma kwa wageni utaongeza mapato ya Halmashauri na upatikanaji wa ajira kwa vijana ndani na nje ya mamlaka ya mji mdogo wa Mombo.

Katika taarifa yake aliyoisoma kwa kiongozi wa huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru,Khalid Nyoni alisema mradi huo umefanikiwa kuwa katika hali nzuri huku akieleza kwamba ndani ya Hotel hiyo kunapatikana  ukumbi wa mikutano,vyumba vya kulala wageni sanjari na uwepo wa huduma za vinywaji na chakula.

Awali akizungumza wakati akipokea Mwenge huo wa Uhuru,mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robert Gabrioel alisema kwamba miradi itakayopitia itagharimu kiasi cha sh. 2,720,871,450/= Bilioni ambapo mwenge utakimbizwa kwenye kilomita 273.5 ukipitia miradi ya maendeleo ipatayo sita.

Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya,Mhandisi Gabriel ni kwamba Mwenge wa Uhuru utapitia miradi hiyo kwa kuiwekea mawe ya msingi,kukaguliwa kuzinduliwa na kufunguliwa ambapo alitaja miradi ya sekta ya utawala,sekta binafsi,sekta ya barabara,sekta ya kilimo,sekta ya mazingira na sekta ya elimu.

Mhandisi Gabriel alisema kwamba miradi hiyo inayotekelezwa Halmashauri ya wilaya imefikia katika hatua mbalimbali za utekelezaji ambapo mmoja umewekewa jiwe la msingi,miradi minne imezinduliwa na mradi mmoja kukaguliwa huku gharama za miradi yote ikiwa kiasi cha sh 939,160,250.
Mwisho.
Pichani wa kwanza mkuono wa kushoto ni mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robart Gabriel akifuatiwa na mbunge wa jimbo la Korogwe mji,Mery Chatanda,akifuatiwa na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Korogwe mji,Jumanne Shauri,mwenyeki wa halmashauri hiyo,Hilaly Ngonyani,viongozi wa CCM wilayani hiyo,eneo la shule ya msingi Kilole wakimsikiliza kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa(hayuko pichani).
Pichani ni St. wa Kwamndolwa akiwasilisha taarifa ya shamba la miti.

Pichani mkono wa kulia ni mkuu wa wilaya ya Korogwe,akimkabidhi mwenge wa uhuru mkurugenzi wa halmashauri ya Korogwe mji,Shauri mkono wa kushoto mara baada ya kukabiziwa na mkurugenzi wa halmashauru ya Korogwe vijijini.
Pichani mkono wa kushoto ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Amour mara baada ya kuwasili wilaya ya Muheza akisalimiana na madiwani wa halmashauri hiyo eneo la Kilulu.
Pichani ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru,Amour mara baada ya kukabidhi hundi ya million moja akiongoza harambee ya upatikanaji wa fedha kijiji cha Lusanga kufanikisha ujenzi wa hospital ya wilaya..
Pichani mkono wa kulia ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2017 kitaifa,Amour mara baada ya kuwasili wilyani Muheza akimsalimia katibu wa CCM wilayani hapo,Mohamed Moyo kulia ambaye amevaa miwani na kofia.

Picha mkono wa kulia ambaye ameshika mwenge wa uhuru ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Handeni vijijini,William mara baada ya kukabiziwa na kaimu mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robart mkono wa kushoto.
Pichani mkono wa kulia ni mkurugenzi wa Handeni mji,Kenneth Haule mara akimkabizi mwenge wa uhuru mkurugenzi wa halmashauri ya Handeni vijijini,William.
Pichani mkono wa kulia ni mkurugenzi wa Handeni mji,Kenneth Haule mara akimkabizi mwenge wa uhuru mkurugenzi wa halmashauri ya Handeni vijijini,William.
Pichani ni mkuu wa wilaya ya Korogwe,Mhandisi Robart akiwahutubia wananchi.

NA SOPHIA WAKATI,HANDENI
KAIMU mkuu wa wilaya ya Handeni,Mhandisi Robert Gabriel amewataka wanafunzi wa sekondari ya Misima kutumia muda mwingi kusoma kwa bidii ili kutimiza ndoto zao maishani. 

Mhandisi Gabriel ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Korogwe alitoa rai hiyo jana alipokuwa akizungumza kwenye sherehe za mwenge wa Uhuru wilayani humo mbio ambazo zilizunguka halmashauri ya Handeni mji kabla ya kwenda vijijini.. 

Katika shughuli hiyo Mhandisi Gabriel aliwaeleza wanafunzi hao kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha yao hivyo wana kila sababu kuzingatia masomo wakiepuka vishawishi na mambo yasiyo ya lazima. 

"Wanafunzi ni vyema mkatumia fursa zilizopo kuzingatia elimu kwa kuwa elimu ndio kila kitu"alisema Kaimu mkuu huyo wa wilaya ya Handeni mkoani Tanga"Mhandisi Gabriel. 

Aidha alitumia nafasi hiyo kumhakikishia kiongozi huyo wa mbio za Mwenge Amour Hamad Amour kwamba maagizo aliyoyatoa yatafanyiwa kazi kwa ustawi wa maisha ya wananchi. 

Awali Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Amour Hamad Amour wakati akikagua mradi wa nyumba za walimu alihoji majengo hayo kuwekwa sakafu ya kisasa 'Tiles ' kuendana na ubora wa nyumba. 

"Mkandarasi hapa imekuaje mbona hakuna 'Tiles' ,imekuaje ujenzi wenu yaani fedha mlizozipata hazikuweza kununua vigae kuboresha hili jengo "alisema Amour ambaye ni kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa. 

Akizungumzia zaidi ujenzi wa nyumba ya walimu ambayo imekamilika katika sekondari ya Misima iliyopo halmashauri ya Handeni mji,kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa,Amour Hamadi Amour alisema itasaidia kuongeza ufanisi.

Aliwataka walimu kuishi kwenye nyumba hizo ili kuwa jirani na eneo lao la kazi hatua ambayo itasaidia kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi wanaosoma shuleni hapo. 
Mwisho.



Pichani ni baadhi ya askari wa FFU wakimbiza mwenge wa uhuru kiomkoa,
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Amour akipanda mti wa kumbukumbu.
Katikati pichani ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Amour akiwahutubia wananchi wa Kwamndolwa wilayani Korogwe.
Huu ni miongoni mwa miradiambayo ilimridhisha kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Amour iliyopo wilayani Korogwe mkoani Tanga.
Pichani ni kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa,Amour akiwa kwenye moja ya mikutano yake ya kuwahutubia wananchi wilayani Korogwe.
Viongozi mbalimbali wakifuatilia ujumbe wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa.



Makabidhiano ya mwenge wa uhuru wilayani Korogwe.

No comments:

Post a Comment