Tuesday 22 August 2017

ZIARA YA SIKU TANO YA RAIS DK.JOHN MAGUFULI MKOANI TANGA ILIKUWA HIVI,,,


Pichani ni rais Dkt.John Pombe Magufuli akiwa katika ziara yake ya siku tano mkoani tanga akiwahutubia wananchi. 

NA SOPHIAWAKATI,TANGA
RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amemtaka Waziri wa viwanda Charles Mwijage kuto kuwafumbia macho dhidi ya wawekezaji wasioendeleza viwanda walivyouziwa badala yake amemuagiza kuwanyang'anya na kugaiwa kwa watu wengine. 

Aliyasema hayo jana alipokiwa kwenye ziara yake ya kutembelea baadhi ya viwanda Jijini Tanga akitanabaisha kwamba hapo awali nchi ya Tanzania ilichezewa kwa watu kuuziwa viwanda kwa mtindo wa kufahamiana huku wakikosa kuviendeleza hivyo kuleta hasara. 

Mbali na kutoa maagizo hayo kwa waziri Mwijage, Rais Dk. Magufuli alimpongeza mwekezaji wa kiwanda cha saruji Kilimanjaro kwa kutoa ajira 180 huku akielezea kuridhishwa na GBP kutoa ajira 1000 sanjari na Tanga Fresh kuwezesha wafugaji 6000 kuuza maziwa na kuweka mkakati wa upanuzi wa kiwanda chao. 

Alipokuwa akizungumzia suala la wawekezaji wasioendeleza viwanda kunyang'anywa Rais Dk. Magufuli alisema utaratibu uliotumika kuvitoa viwanda hivyo alioueleza kuwa wa kirafiki umeua viwanda vingi hadi Korona za mashamba ya mikonge ambazo ni mali ya watanzania. 

Alisema kwamba lengo la serikali kujenga viwanda ni ili kupata kodi na wananchi wake waweze kupata ajira jambo ambalo halikuweza kuonekana katika kipindi kirefu. 

Katika taarifa yake kwa Rais meneja wa kiwanda cha Tanga Fresh,Michael Karata alisema licha ya kufanikiwa kutoa ajira kwa asilimia 42 wananchi ni wabia wa kiwanda hicho cha maziwa. 

Aidha Karata alisema wanakabiliwa na changamoto huko TRA walikokwenda kusajili hati walitozwa faini jambo ambalo limekuwa kikwazo kwao katika kufanya upanuzi wa kiwanda chao. 

Rais Dk.Magufuli katika majibu yake juu ya changamoto hiyo alisema kwa kuwa Tanga Fresh ni watu wa tatu kununua kiwanda hicho hawapaswi na deni hilo badala yake ameagiza Azania kubanwa walipe fedha hizo husika. 

Kabla ya Rais kutoa kauli hiyo waziri Mwijage alimweleza kuwa Tanga Fresh ilipofika hapo ilikuwa ni mkono wa tatu baada ya kuachiwa na kampuni ya Azania. 

Katika ziara hiyo ambayo Rais Dk. John Magufuli alitembelea viwanda alisema sura ya Tanga iliyopotea miaka 20 iliyopita imeanza kurejea huku sababu kuu ya kufa kwake akiitaja kuwa ni baadhi ya wawekezaji wasioitakia mema Tanga kutoviendeleza. 

Alisema wawekezaji hao walidiriki kujipatia fedha kwenye taasisi mbalimbali na kwenda kuwekeza maeneo mengine huku akisisitiza kusema kuwa hadhi ya uchumi mkoani Tanga imeanza kurejea. 
Mwisho. 


Picha ni rais Dk.John Magufuli akiwa kwenye moja ya ziara yake ya kutembelea viwanda viwand vitatu,akiwa kituo cha mafuta GBP jijini Tanga.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
RAIS Dk. John Pombe Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na baadhi ya wawekezaji ambao wameshindwa kuendeleza viwanda akisema wameshindwa kuitendea haki serikali ya Tanzania. 

Hata hivyo,amesema kuwa wawekezaji wa aina hiyo wamesababisha miongoni mwa viwanda 72 hapa nchini kufa huku vichache vikiendelea kujikongoja kwa uzalishaji bidhaa mbalimbali. 

Kauli hiyo ameitoa juzi wakati akiweka jiwe la ufunguzi kiwanda cha kuzalisha Saruji Kilimanjaro huku akimuagiza waziri wa viwanda,Charles Mwijage kuchukua hatua dhidi ya viwanda vilivyoshindwa kuendelezwa. 

Akionyesha msisitizo juu ya hatua yake hiyo ya kumuagiza waziri Mwijage,Rais Dk. Magufuli akitolea mfano kwamba hata mwenzake waziri,William Lukuvi ameweza kuorodhesha mashamba yote yasiyoendelezwa na kufutiwa hati. 

Akihimiza uwepo wa viwanda vya ndani Rais Dk. Magufuli alimtaka waziri huyo,Mwijage kufuatilia nchi jirani kuhakikisha kuna bidhaa za Tanzania yakiwemo maziwa akisema kama itajitokeza kukataliwa kuuza basi nao wasiuze hapa nchini. 

Rais Dk. Magufuli alisema kuwa awali nchi ilikuwa na viwanda 197 lakini kuna baadhi ya watu wamevichukua kwa bei nafuu sawa na bure huku wakienda kudiriki kukopa fedha ndani na nje ya nchi na kuvitelekeza. 

"Baadhi ya wawekeza hawakuitendea haki Tanzania na kupelekea kubaki na viwanda 11 Afrika huku vingine vikijikongoja kwa uzaliahaji "alisema Rais Dk Magufuli. 

Kwa upande wake meneja masoko kiwanda cha Kilimanjaro,Hashim Hafidhi alisema kiwanda hicho kimeanzishwa 2013 kwa kuanza na wafanyakazi 40 ambapo sasa ajira zilizotolewa ni 189 kwa kutoa mafunzo kama teknolojia ya umeme. 

Vilevile Hafidhi alisema kuna changamoto mbalimbali zinazowakabili akishauriwa kupunguziwa mzigo wa kodi japo kwa miaka kumi kutokana na kiwanda hicho kuwa kipya huku kukiwa na saruji kutoka Pemba na Unguja kunusuru soko la ndani. 

Mwisho. 

Pichani ni viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri wakijibu hoja mbalimbali kwenye ziara hiyo ya rais.



No comments:

Post a Comment