Thursday 19 October 2017

UCHAGUZI NDANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM ULIKUWA HIVI KOROGWE,,

 Pichani ambaye ameshika kipaza sauti ni katibu wa CCM Korogwe mjini akitoa maelekezo kwa wajumbe.
 Pichani ni katibu wa CCM halmashauri ya Korogwe mjini akitoa maelekezo kabla ya uchaguzi kwa wajumbe halali wenye sifa ya kupiga kura.
 Pichani ni baadhi ya wajumbe wa halmashauri ya Korogwe mjini mara baada ya kukamilisha zoezi la kupiga kura wakisikiliza matokeo ukumbi wa halmashauri hiyo.
Pichani ambaye amesimama kashika kipaza sauti ni msimamizi wa uchaguzi halmashauri ya Korogwe vijijini,Dastan Kitandula ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Mkinga mkoani Tanga,akitangaza matokeo ukumbi wa chuo cha ualimu wilayani hapo.


MKUTANO mkuu wa uchaguzi kwa Chama cha map[induzi CCM Korogwe Mjini umefanyika jana kwenye ukumbi wa halmashauri ya Mji ambapo Kada Mwenyekiti Emmanuel Chale amefanikiwa kutetea vyema wadhifa wake baada ya kuwabwaga wanachama wengine wawili waliokuwa wakiwania kiti hicho.

Katika kinyang’anyiro hicho cha nafasi ya mwenyekiti Chale aliyepata kura 205 alikuwa akichuana na Iddi Sad Mdoe na Athuman Magogo  ambapo kwa nafasi ya mkutano mkuu wa Taifa wagombea walikuwa tisa (9) huku Dk Frank Mhilu,Mjata Daffa na Asia Kingongo wakipata wasaa wa kuwa wawakilishi.

Uchaguzi huo pia ulihusisha upatikanaji wa nafasi za wajumbe kutoka vijana kwenda halmashauri kuu ambao walipita bila kupingwa ni Ally Chamzimu,Mujibu Salim,Muntalla Mkesa na Pascal Itemo wakati Anna Kanyika,Mariamu Lyagoda na Rose Magembe walifaniweza kuwa wajumbe kwenda UWT.

Mbali na nafasi hizo pia uchaguzi huo ulimchagua mwanaharakati wa masuala ya mazingira Revocatus Njau kuwa katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi CCM Korogwe Mjini akifanikiwa kuwabwaga wenzake watatu huku Elizabeth Haule na Allen Kingama wakitwaa nafasi ya mkutano mkuu mkoa.

Walioshinda nafasi ya halmashauri kuu kwenda wazazi ni Thobias Nungu na Raphael Mbughuni ambapo mara baada ya matokeo hayo yote kutangazwa mwenyekiti wa CCM wilaya aliyechaguliwa Emmanuel Chale alitumia fursa hiyo kuwasihi wanachama kuimarisha mshikamano ili kuweza kujenga chama chao.

Chale alisema kuwa ili kuweza kuimarisha chama chao kwa kuondosha makundi huku akisistiza kusema kuwa uchaguzi ulishamalizika na sasa kila mwanachama anapaswa kutumia mafasi aliyonayo kukitumikia chama kwa maslahi ya umma akisema kwa pamoja wanapaswa kumuunga mkono Rais kuchapa kazi.

Wakati Korogwe Mjini wakihitimisha uchaguzi huo nako Korogwe vijijini kwenye ukumbhi wa chuo cha Ualimu TTC kulifanyika uchaguzi wa aina hiyo uliomwezesha Hemed Nassoro ‘Malingumu’ kunyakua nafasi ya mwenyekiti akifanikiwa kumbwaga kwa mbali kada wa chama hicho tawala Rajabu Kaniki.

Katika kinyang’anyiro hicho cha wadhifa wa Mwenyekiti Malingumu alitetea nafasi yake hiyo kwa kupata kura 745 wakati Kaniki akipata 141 na kwa nafasi ya katibu mwenezi aliyefanikiwa kushika wadhifa huo ni Ally Waziri kwa kura 98 akiwa miongoni mwa wanachama waliofanikiwa kutetea nafasi zao za awali.

Wazi alikuwa akichuana na Bakari Rashidi aliyepata kura 10,Peter Mfumya kura 10 na Salimu Mhando kura moja uchaguzi ambao ulilazimika kurejewa mara ya pili baada ya kujitokeza mkanganyiko kwa kura kudaiwa kuongezeka katika hatua za awali kwa mafasi hiyo ya kumpata mwenezi wa chama hicho.

Akizungumza mara baada ya uchaguzi huo kumalizka mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Korogwe Vijijini Hemed Nassoro ‘Malingumu’ alisema CCM ya mazoea imepitwa na wakati na hata ile iliyokuwa ikionekana kuwa legelege ama ya makundi haipaswi kuendelea kuwepo zaidi ya kuchapa kazi.

Aliwataka wanachama wa chama hicho tawala kuelekeza nguvu zao katika uchaguzi wa serikali za mitaa hapo mwaka 2019 na uchaguzi mkuu wa madiwani,ubunge na Rais kwa mwaka wa 2020 akisisitiza kusema kuwa kuna kila sababu kwa CCM kuendelea kushika dola kwa maslahi ya watanzania wote.
Mwisho.


No comments:

Post a Comment