Monday 16 April 2018

MAADHIMISHO YA WIKI YA BANDARI ILIKUWA HIVI MKOANI TANGA,,

 Pichani katikati ni mkuu wa mkoa wa Tanga,Martin Shigela akizindua boti mpya ya kisasa iliyotolewa na serika ambayo imegharimu sh.billion nne za kitanzania  kwa ajili ya ulinzi mizigo ya magendo bahari ya Hindi, juzi miongoni mwa shughuli zilizofanyika
wiki ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa TPA kwa sheria namba 17 ya mwaka 2004 ya usimamizi wa Bandari.na kushoto ni Meneja wa bandari mkoa wa Tanga,Percival Salam

 Wadau wa bandari mkoani Tanga wakiwa kwenye kikao
 Pichani ni boti mpya ya kisasa ya ulinzi iliyogharimu sh.billion nne za kitanzania  kwa ajili ya ulinzi mizigo ya magendo bahari ya Hindi, juzi miongoni mwa shughuli zilizofanyika katika.
wiki ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa TPA kwa sheria namba 17 ya mwaka 2004 ya usimamizi wa Bandari.


 Pichani ni Meneja wa bandari mkoa wa Tanga,Percival Salama mara baada ya kamilika kwa zoezi la michezo wakijipongeza kwa pamoja.

Pichani ambaye ametangulia ni Meneja wa bandari mkoa wa Tanga,Percival Salama akiwa ameambatana na wafanyakazi na wadau wa habari Siku ya kuhitimisha sherehe ya wiki ya bandari miaka 13 tangu kuanza kutoa huduma.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MAMLAKA ya usimamizi wa bandari mkoani Tanga TPA,imesema ina mpango mkakati wa kuhudumia kiasi cha shehena ya mizigo tani millioni 2 kwa mwaka ifikapo mwakani baada ya kuwasili kwa mashine mpya za kupakua na kupakia mizigo melini.

Meneja wa bandari mkoa wa Tanga,Percival Salama alisem kwamba katika utekelezaji wa wa ahadi ya rais Dk.John Pombe Magufuli kuna mashine mbili za kisasa zinatarajiwa kuwasili nchini mwezi Machi na zitafungwa kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma katika bandari hiyo.

Alisema kwamba pia hivi sasa uwezo wa bandari hiyo ni mkubwa kuhudumia shehena ya mizigo kiasi cha tani 750,000 kwa mwaka kutoka tani 548,000 katika kipindi cha mwaka 2015 kuhudumia shehena hiyo.

Meneja huyo alitaja mafanikio ya uhudumiaji mizigo kwa bandari hiyo tangu mwaka 1960 ambapo waliweza kuhudumia shehena ya mizigo ipatayo tani 212,000 ilipanda na kufikia tani 380,000 mwaka 1975.

"Kiukweli sasa tunafanya maboresho ya uhakika katika bandari yetu, kwa kufunga mashine mpya mbili za kushusha mizigo na kupakia melini lakini pia tutakuwa na Tag zitakazoweza kubeba tani 100 kwa wakati mmoja," alisema meneja huyo Salama.

Aidha abainisha kueleza kwamba uwepo wa bandari ya Tanga inaumuhimu mkubwa kwa ukuaji wa uchumi mkoani humo na pia ni fursa nzuri kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kupitisha mizigo yao kwa kuwa inahudumiwa katika muda mfupi kuliko bandari yoyote hapa nchini.

Salama alitaja miongoni mwa nchi ambazo zinaweza kuhudumiwa moja kwa moja na bandari hiyo kuwa ni ile ya Zambia, Malawi, DR Congo, Rwanda, Burundi, Uganda na nchi jirani ya Kenya kupitia miundombinu bora ya reli na barabara.

Mkuu wa wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Tanga,Martin Shigela katika uzinduzi wa wiki ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa TPA kwa sheria namba 17 ya mwaka 2004 ya usimamizi wa Bandari.

Alisema kwamba aliipongeza bandari hiyo kwa jitihada za kuongeza ufanisi mzuri wa kazi wanaofanya katika kuhudumia shehena za mizigo na ushirikiano na vyombo vyengine vya dola udhibiti suala la magendo kwa njia ya bahari.

"Mamlaka ya bandari maboresho mnayoyafanya yana mchango mkubwa kwa maendeleo ya nchi, na hii ndiyo maana serikali kuu imekuwa ikitoa fedha lengo kuhakikisha uboreshaji unafanyika," alisema DC Mwilapwa.

Mkuu huyo wa wilaya alisema jitihada zinazofanywa na bandari hiyo katika kudhibiti bidhaa za magendo zinazopita katika bandari bubu zilipo kwenye mwambao wa bahari ya Hindi na akaahidi mkoa umeanza kuchukua hatua kupambana na magendo.

"Mkuu wa mkoa ameagiza kwamba zilebidhaa za  shehena ambazo tutakuwa tunakamata na chombo zaidi ya Mara tatu magendo itabidi viongozi wa maeneo hayo watakuwa hawatoshi kuwepo,baada ya kujiridhisha wawajibike," alisema Mwilapwa.

Pia alitoa wito kwa watu wanaotaka kuwekeza katika Jiji la Tanga kwamba maeneo bado yapo na Halmashauri tayari imetenga eneo la Pongwe kwa ajili ujenzi wa viwanda mbalimbali.
Hata hivyo,katika uzinduzi huo wa wiki ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa TPA kwa sheria namba 17 ya mwaka 2004 ya usimamizi wa Bandari wamefanikiwa kuchangia Uniti 27 za damu kusaidia wagonjwa wenye mahitaji katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment