Tuesday 17 April 2018

KANISA LA WADVENTIST WASABATO KANA LATOA MSAADA WA MASHUKA 232 KUSAIDIA WAGONJWA HOSPITALI YA MKOA BOMBO KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI,,

 Pichani ni Mchungaji wa kanisa la Wadventist Wasabato wa mtaa wa Kana Jijini Tanga, Jackson Mdingi, ofisini kwake akizungumza na waandishi hawapo pichani,lengo la kutoa msaada wa mashuka 232 katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo ni baada ya kuguswa na utendaji kazi mzuri wa rais wa awamu ya tano Dkt.John Pombe Magufuli.
 Pichani ni vijana, watoto wa kanisa la Wadventist Wasabato wa mtaa wa Kana Jijini Tanga,maarufu WATAFUTA njia wakiwa na viongozi na Mchungaji wao, Jackson Mdingi, katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo katika zoezi la kukabidhi mashuka 232 baada ya kuguswa na utendaji kazi wa rais Dk.John Magufuli.
 Picha zote ni vijana, watoto wa kanisa la Wadventist Wasabato wa mtaa wa Kana Jijini Tanga,maarufu watafuta njia wakiwa na viongozi na Mchungaji wao, Jackson Mdingi, juzi katika hospitali ya mkoa wa Tanga Bombo katika zoezi la kukabidhi mashuka 232 baada ya kuguswa na utendaji kazi wa rais Dk.John Magufuli.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
TAASISI na Mashirika ya dini nchini yameombwa kusaidia jamii kwa njia mbalimbali ikiwemo sekta za afya, elimu na mazingira kama mchango wa kuunga mkono jitihada za serikali zinazofanywa na Rais dK.John Magufuli za kujenga uchumi kwa kutumia rasilimali zilizopo.

Wito huo umetolewa na Mchungaji wa kanisa la Wadventist Wasabato wa mtaa wa Kana Jijini Tanga, Mch Jackson Mdingi, alipokuwa akikabidhi mashuka 232 kwa ajili ya matumizi ya wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tanga, Bombo yenye thamani ya sh. 2,552,000.

Alisema msaada huo wa mashuka wametoa baada ya kuhamasika na jitihada zinazofanywa na Rais Magufuli katika kujenga nchi kwa kutumia rasilimali hivyo wakaona ni vema wakasaidia nao kutoa huduma za kijamii kama mchango wao kwa serikali.

"Kiukweli sisi kanisa la Wadventist Wasabato tunaunga mkono jitihada anazofanya Rais za kuijenga nchi kwa rasilimali yetu, hivyo tunatoa wito kwa taasisi na mashirika ya dini tuiunge mkono serikali kwa kazi wanazozifanya kuwasaidia waumini wetu," alisema mchungaji huyo Mdingi. 

Alisema kama kanisa limetoa mashuka hayo ambapo ni utaratibu wa kusaidia jamii katika mambo mbalimbali ikiwa ni miongoni mwa jitihada za kuunga mkono kazi zinazofanywa na serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya na Elimu.

Mchungaji huyo alibainisha kuwa taasisi za dini zinapounga mkono jitihada za serikali katika huduma mbalimbali kwa sekta zenye mahitaji kutawasaidia wananchi kuweza kupunguza malalamiko kuhusu huduma zinazotolewa.

Alisema serikali ya awamu ya Tano tangu iingie madarakani imekuwa ikijitahidi kujenga nchi kwa kutengeneza miradi mikubwa kwa kutumia fedha za nchi hatua ambayo inapaswa kuungwa mkono na Watanzania wote bila kuingiza itikadi ya kisiasa.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment