Tuesday 24 April 2018

AJALI YA LORY KUACHA NJIA NA KUGONGANA USO KWA USO NA GARI LA POLISI NA KUSABABISHA KIFO CHA ASKARI NA MAJERUHI WANNE,,

 Pichani ni Kamanda wa polisi mkoani Tanga Kamishina Msaidizi wa Polisi (SACP),Edward Bukombe akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) sakata la ajali iliyotokea saa 7:30 mchana baada ya gari la polisi aina ya land Rover Lenye namba PT 1503 kugongana uso kwa uso na lory la mizigo.
 Pichani ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu Msaidizi wa polisi (ASP),Sadick Msangi,akikagua gari la polisi aina ya land Rover Lenye namba PT 1503 kugongana uso kwa uso na lory la mizigo mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo na kulifikisha kituo cha mabawa trafick likiwa gereji.

 Pichani ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu Msaidizi wa polisi (ASP),Sadick Msangi,akikagua gari  lory la mizigo lenye namba T142 DCA likiwa na tela lenye namba T802 DMW mara baada ya ajali hiyo kutokea likiwa kituo cha trafick mabawa trafick.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
ASKARI wa Kitengo cha Upelelezi mwenye namba za polisi E 8726 Sajenti Henri amefariki dunia na wenzake wanne kujeruhiwa vibaya katika ajali iliyohusisha gari la polisi walilopanda kugongana uso kwa uso na lory la mizigo iliyotokea eneo la Chumvini barabara kuu ya Horohoro Jijini Tanga.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga Kamishina Msaidizi wa Polisi (SACP),Edward Bukombe alisema kwamba ajali hiyo ilitokea juzi  saa 7:30 mchana baada ya gari la polisi aina ya land Rover Lenye namba PT 1503 kugongana uso kwa uso na lory.

Alisema marehemu alikuwa amepanda gari hilo la polisi lililokuwa doria za kawaida lililokuwa likiendeshwa na  polisi mwenye namba G 2416 Konstebo Barnaba, likiwa na askari wengine watatu waliokuwa wakitoka Horohoro, ghafla waligongana na lory hilo lenye namba T142 DCA likiwa na tela lenye namba T802 DMW.

“Askari wetu walikuwa wakirudi doria kutokea njia ya Horohoro, mara ghafla lory likaacha njia likawafuata upande wao na kuwagonga na kwavile gari letu lilikuwa dogo liliwaumiza vibaya askari wote wakakimbizwa katika hospitali ya mkoa Bombo kwa ajili ya matibabu zaidi,” alisema kamanda Bukombe.

Kamanda huyo alisema kuwa marehemu ambaye alikuwa ameumia vibaya eneo la kichwani ambapo alifariki saa 10:06 jioni akiwa anapatiwa matibabu katika hospitali ya Bombo na kwamba hivi sasa askari wengine wanaendelea kupatiwa matibabu.

Aliwataja askari hao wa kitengo cha upelelezi wanaoendelea na matibabu katika hospitali ya Bombo kuwa ni pamoja na dereva ya polisi ambaye ameruhisiwa waliobaki ni watatu kuwa ni polisi wa kike WP 9787 Fatuma, G 2200 Konstebo Jafari na G 2066 Konstebo Obedi.

Kamanda Bukombe alisema kwamba dereva wa lory mara baada ya kusababisha ajali hiyo alikimbia na hadi sasa bado hajapatikana na jeshi hilo kwa kushirikiana na mmiliki wa gari hilo wanaendelea kumtafuta ili aweze kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Nae Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu Msaidizi wa polisi (ASP),Sadick Msangi, aliwatahadharisha madereva kuwa makini barabarani kutokana na kwamba wanapokiuka sheria za usalama barabarani husababisha vifo au kuwapa ulemavu watu wasiohusika.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment