Monday 7 May 2018

SAKATA LA BABA KUMPA MIMBA BINTI YAKE WA KIDATO CHA TATU SHULE YA SEKONDAR MKATA WILAYANI HANDENI,,,

NA SOPHIA WAKATI,HANDENI 
POLISI kwa kusirikiana na raia wema wamemkamata Yahaya Juma (48) mkazi wa Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga,akituhumwa kumpa mimba binti yake ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha tatu.

Afisa tarafa wa tarafa ya Mazingara wilayani Handeni,Hashimu Msagati ametoa taarifa hiyo juzi wakati akizungumza na Gazeti hili wilayani Handeni mkoani Tanga.

Afisa huyo alisema,mtuhumiwa alimpatia ujauzito huo binti yake katika kipindi cha mwaka jana akiwa kidato cha pili ambapo ameshajifungua mtoto wa kike.

Alisema mtuhumiwa huyo,Juma baada ya kutenda tukio hilo alikimbia kusikojulikana lakini wananchi waliweka mtego ambapo Mei 3 mwaka 2018 alionekana kwenye kijiwe cha kahawa akiwa amepumzika na jamaa zake.

Msagati aliongeza kusema kuwa baada ya wananchi kumuona ndipo walitoa taarifa kwake na kituo cha polisi Mkata ambapo waliambatana na askari wa kituo hicho Edwin Msiba na hivyo kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo mganga wa kienyeji.

"Huyu bwana alitoroka ndio sababu tulichelewa kumkamata,binti yake amemtaja alipoenda hospitali kujifungua baada ya kutishwa na manesi kukosa kupewa huduma iwapo hatamtaja aliyempa mimba" alisema Msagati.

Aidha Msagati alisema mtuhumiwa huyo anaelezwa kuwa hii ni mara ya pili kuzaa na binti zake ambapo yupo mkubwa aliyezaa naye hivi sasa yupo tayari kutoa ushahidi mahakamani.

Kamanda wa polisi mkoani Tanga,Edward Bukombe amethibitisha kutokea kwa tukio hilo akisema ni kweli katika kituo cha Mkata anashikiliwa,Juma Yahaya miaka 48 mkazi wa Mkata ambaye ni mganga wa kienyeji.

Alisema kwamba mtuhumiwa anashikiliwa akidaiwa kumpatia mimba mwanae wa kidato cha tatu aliyekuwa akisoma kidato cha tatu shule ya sekondari Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga.

Amesema mtuhumiwa katika mahojiano na jeshi la polisi amekataa lakini anaendelea kushikiliwa na baada ya uchunguzi kutoka maeneo mbalimbali kukamilika atafikishwa mahakamni ili kukabiliana na tuhuma inayomkabili.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment