Sunday 20 May 2018

KANISA LA WAADIVENTIST WASABATO WAKITUMIA FUTARI KUIMARISHA NA KUONYESHA UPENDO NA UMOJA WA TAIFA AMBAO ULIASISIWA NA WAASISI WALIOPITA,,,

 Pichani ni viongozi wakibadilishana mawazo baada ya kukamilisha zoezi la futari.
 Pichani ni Shehe wa mkoa wa Tanga (BAKWATA),Sheikh Mohammed Luwuchu akimshukuru mchungaji Mdingi akielezea ni kiongozi wa dini mkoani Tanga wa kipekee ambaye mara nyingi ameonesha kujitoa katika mambo ya kulinda na kuenzi amani ya nchi.
 Pichani aliyevaa kazu na koti jeusi ni mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa mara baada ya futari akiteta kitu na mwandishi wa gazeti la Tanzania Daima ambaye ni muumini wa msikiti huo.
 Pichani ni baadhi ya waumini wakiwa kwenye zoezi la futari.
Pichani mkono wa kushoto ambaye amevaa koti jeusi na miwani Mchungaji wa Kanisa la Waadiventist Wasabato lililopo Kana Jijini Tanga, Jackson Gladson Mding" wakiwa nje ya msikiti wa Majengo Kona baada ya hafla ya kufuturisha akiongena na mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa aliyevaa kazu na koti jeusi katikati akifuatiwa na kamanda wa polisi mkoani hapo.mkono wa kulia.



NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MCHUNGAJI wa Kanisa la Waadiventist Wasabato lililopo Kana Jijini Tanga, Jackson Gladson Mding" amesema ataendelea kuimarisha na kulinda amani iliyoasisiwa na waasisi wetu nchini kwa mshikamano, upendo na umoja wa Kitaifa.

Kauri hiyo ameitoa juzi wakati akizungumza katika futari iliyoandaliwa na kanisa lake na kuwafuturisha Waislamu wa msikiti wa Mapinduzi Kona Jijini hapo, Mchungaji Mdingi amesema lengo la kuandaa futari hiyo ni njia mojawapo ya kuendeleza umoja na udugu miongoni mwa Wakristo na Waislamu hapa nchini.

"Kiukweli sisi Wasabato tumeandaa futari hii kudumisha udugu na upendo,kuimarisha na kulinda amani iliyopo na kudumisha mshikamano wa Waasisi wetu ambao walifanya kazi kubwa ya kuijenga nchi katika misingi ya amani,hivyo hatuna budi kuilinda na kuwaombea kwa pamoja," alisema Mdingi.

Aidha,alisema kwamba waumini wote ni ndugu na hawapaswi kubezana kudharauriana kwa vile wapo waliooana na kuchangamana katika dini hizo lakini pia wamekuwa wakishirikiana katika shughuli mbalimbali za kujenga Taifa.

"Sisi tumeoleana na tumeingiliana kwenye mambo mengi tunakutana kwenye shughuli nyingi za kijamii, kwanini kwenye ibada tusichangamane pamoja kama hivi na kuliombea Taifa letu pamoja?" Alihoji mchungaji huyo.

Mchungaji huyo alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa ndugu zao Waislamu washirikiane pamoja katika masuala mbalimbali ya elimu na ujasiriamali ili kuwawezesha waumini wao kuwa na uwezo wa kufanya kazi na kumcha Mungu.

Naye Shehe wa mkoa wa Tanga (BAKWATA),Sheikh Mohammed Luwuchu alimshukuru mchungaji Mdingi kwa kumuelezea ni kiongozi wa dini mkoani Tanga wa kipekee ambaye mara nyingi ameonesha kujitoa katika mambo ya kulinda na kuenzi amani ya nchi.

Alisema mchungaji huyo katika umoja wa kuchangamana pamoja na Waislamu na Wakristo katika masuala mbalimbali hakuna sehemu nyingine nchini yenye mshikamano wa dini zote mbili.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika futari hiyo alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa ambaye alitaka madhehebu mengine ya dini yaige mfano mzuri uliooneshaa na dhehebu hilo la Wasabato.


Mwisho.



No comments:

Post a Comment