Wednesday 13 October 2021

MAADHIMISHO YA JUMA LA WANAWAKE UWT MKOANI TANGA MWAKA 2021 YALIKUWA HIVI,,,,




NA SOPHIA WAKATI,MUHEZA

UMOJA wa Wanawake UWT mkoani Tanga wametakiwa kuhamasisha kina mama kuona umuhimu kujiunga kwenye vikundi ili kuwawezesha kunufaika na mikopo ya halmashauri kujiinua kiuchumi.

Hata hivyo,imeelezwa kwamba elimu hiyo itawezesha kuwasaidia kina mama kurahisisha kufanyabiashara kwa tija na  kusaidia familia zao kiuchumi na taifa kuweza kupiga hatua.

Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa mkoani Tanga,Catherin Kitandula juzi alipokuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya Juma la wanawake wa mkoa wa Tanga shughuli ambayo kimkoa yamefanyika wilayani Muheza.

''Kiukweli kwenye suala la uchumi siku ya Demokrasia ya mwaka huu namnukuu''rais Samia Suluhu Hassan alialikwa  kwenye sherehe ya kupongezwa kuwa mwanaDemokrasia mzuri na kuahidi atakwenda kulisimamia kwa karibu zaidi kuwakomboa wanawake kiuchumi''alisema Catherin.

Mjumbe huyo wa halmashauri kuu ya CCM taifa,Catherin alisema chama cha mapinduzi kinaelekea kwenye zoezi la uchaguzi wa chama hicho kimewataka wanawake kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika ngazi ya wilaya na ikiwezeka hadi mkoa.

Pia alitumia nafasi hiyo kwa kuwataka viongozi wanawake kuendelea kuongeza wanachama wapya kwenye welaya ili kuweza kupata jeshi kubwa la kuleta ushindi ndani ya chama hicho cha CCM. 

''Ndugu zangu kina mama wanajukumu kubwa la kusimamia familia zao ikiwemo nyendo za watoto ili kuweza kuwaondolea vikwazo katika masomo na kuweza kutimiza malengo yao''alisema.

Awali katibu wa UWT mkoa wa Tanga,Sophia Nkupe alisema lizitaja shughuli zilizofanya na wanaCCM hao kupitia jumuiya yao ni usafi na kuona wagonjwa hospitali,kukagua mabweni ya watoto waliopo makundi maalum,kutembelea Magereza mambo ambayo yamefanyika wilaya zote za mkoa wa Tanga.

Alisema kwamba maadhimisho ya wiki ya UWT kwa mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu inayosema kumkomboa mwanamke kiuchumi,kifikra na kisiasa. 

Nkupe alitanabaisha kwamba kupitia maadhimisho hayo wamefarijika kuona Ilani ya CCM imetekelezwa vyema huko shule ya Mbaramo kwenye ujenzi wa mabweni ya watoto wenye ulemavu na pia maboresho yaliyofanyika hospitali yaUbwari Muheza.

Naya Mwenyekiti wa CCM Muheza,Gugu Lack amepongeza wenyeji wa maadhimisho hayo kimkoa ambao ni Muheza akisema wameyafanikisha kwa kiasi kikubwa huku akitilia msisitizo suala la hamasa ya kupatikana kwa wanachama wapya.

Alisema,chama cha mapinduzi CCM hakitaweza kuendelea kushika dola kama hakitakuwa na wanachama wa uhakika akisisitiza uingizwaji wanachama wapya hasa kundi la vijana.

Aidha Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Tanga Dk Aisha Kigoda amewahiza watoto kusoma kwa bidii ili kuja kuwa viongozi wa baadaye huku akiwataka wazazi na walezi kuwasimamia vijana hao kuwawezesha kutimiza ndoto zao.

Maadhimisho hayo pia yametoa wito kwa wanawake kujiunga katika vikundi ili kukopesheka kirahisi hatua ambayo itawawezesha kujianzishia miradi na hivyo kujikwamua kiuchumi.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment