Wednesday, 13 October 2021

MECHI YA KIRAFIKI KATI YA TANESCO TANGA NA TANESCO KILIMANJARO mwaka 2021 ILIKUWA HIVI,,,,,

 

Pichani ni wachezaji wa timu ya Tanesco Tanga baada ya mechi wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wao,,,Tanga na Kilimanjaro Hakuna  Mbabe

 

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

KATIKA kuboresha mahusiano katika maeneo ya Kazi mwishoni mwa wiki kumefanyika Mchuano Mkali wa Soka kati ya Timu ya Tanesco Tanga na ile ya Kilimanjaro ,mchezo ambao ulipigwa kwenye Uwanja wa Shule ya Popatlal Jijini Tanga.

 

Kwenye Mchezo huo wa Kirafiki wa kupimana nguvu Timu hizo zilitoka Uwanjani nguvu sawa zikiwa zimefungana bao moja kwa moja huku Tanasco Tanga ikifanikiwa kuongoza katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

 

Wakati timu hizo zikienda mapumziko huku Tanesco Tanga wakiongoza, wapinzani wao Tanesco Kilimanjaro katika dakika 45 za kipindi cha pili walikuja na nguvu mpya na kufanikiwa kusawazisha bao hilo na wenyeji wao.

 

Kwa upande wa Tanesco Tanga goli lao lilifungwa kunako dk ya 33 kwa mkwaju wa adhabu ndogo uliopigwa na Mshambuliaji wao Sebiga Sebiga baada ya Wapinzani wao kucheza ndivyo sivyo hadi kupelekea kuadhibiwa.

 

 

Goli la kusawazisha la Tanesco Kilimanjaro lilifungwa katika dakika ya 71  na Mshambuliaji machachari Omari Msuya aliyemalizia mpira uliomponyoka mlinda mlango wa Tanesco Tanga na hivyo timu hizo kutoka Sare ya 1 kwa 1.

 

Mwisho.

No comments:

Post a Comment