Picha zote ni kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Tanga,Safia Jongo jana ofisini kwake huku akiwaonye waandishi wa habari jezi feki 227 zilizokamatwa kwenye operesheni.
Picha na Sophia Wakati,Tanga
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
JESHI la polisi mkoani Tanga limefanikiwa kukamata jezi feki za klabu ya Simba 227 katika operesheni inayoendelea katika maduka mbalimbali,bila ya kulipa ushuru ambapo imeelezwa kuwa ni sawa na Wahujumu Uchumi
Alisema tukio hilo lilitokea juzi katika maduka mbalimbali jijini Tanga na kubaini wamezipata kinyume na sheria huku zikiwa zinauzwa bila nyaraka muhimu za serikali.
Jongo alikuwa akizungumzi operesheni maalum iliyofanywa na Jeshi la polisi na
kampuni ya Vunjabei Group Ltd waliyoingia mkataba wa kuzalisha Jezi za
klabu ya Simba yenye masikani yake jijini Dar es Salaam.
Kamanda Jongo ameasa vitendo vya baadhi ya wafanyabiashara kujihusisha
na uingizaji na uuzaji jezi feki akisema huo ni uhujumu uchumi kwa
kuwa hawalipi ushuru hivyo wanaikosesha mapato Serikali.
Kwa upande wake meneja wa masoko wa kampuni ya Vunjabei Group Ltd,
Fadhili Fabian Ngajilo wamepata mkataba wa kuzalisha jezi za klabu ya
Simba kwa msimu wa mwaka huu na ujao.
Hata hivyo amesema,kumezuka watu wanaozalisha jezi zinazofanana na zao
jambo ambalo ni kinyume cha taratibu na sheria ambapo tayari
operesheni imeanza nchi nzima kuwanasa wafanyabiashara hao.
Amelipongeza jeshi la polisi mkoa wa Tanga kwa ushirikiano katika
kuwasaka wafanyabiashara hao ili hatua za kisheria kuweza kuchukuliwa
dhidi yao.
Amebainisha kuwa wafanyabiashara hao wanaoingiza jezi feki wako katika
makundi matatu na tayari watu kadhaa huko Dar es Salaam wanashikiliwa
huku uchunguzi ukiendelea ili hatua zaidi kuchukuliwa.
Kwa mujibu wa meneja masoko huyo kundi la kwanza la wafanyabiashara
hao ni wale wanaoingiza jezi feki nchini baada ya kuzalisha.
Wengine ni wafanyabiashara wenye maduka wanaonunua kwa wale
wanaoingiza ikiwa ni pamoja na wamachinga ambapo wote wanahusishwa na
uuzaji jezi feki za Simba.
Meneja huyo amesisitiza kusema kuwa iwapo mtu atahitaji jezi ya Simba
vyema akawasiliana na klabu husika ama kampuni ya Vunjabei Group
Limited.
Ameendelea kusema kuwa kampeni ya kuwasaka watu hao wanaofanya hujuma
kwa kuzalisha na kusambaza jezi za kughushi haitapoa na inaendelea
nchi nzima.
Pamoja na hayo ametaka wenye jezi feki kuzisalimisha polisi au
kuziteketeza kwa kuzichoma moto huku akiwasihi wanunuzi binafsi
kuhakikisha wananunua bidhaa halisia.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment