Pichani ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri KKKT Usharika wa Kana Dayosisi ya KaskaziniPwani, Masharik Ketto
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
KANISA la Kiinjili la Kilutheri KKKT
Usharika wa Kana Dayosisi ya
Kaskazini Mashariki limewataka Watanzania
kuendelea kumrudia Mungu
hatua ambayo itawawezesha kuwa na mafanikio
katika mwaka huu mpya wa 2022.
Hata hivyo,pia amewata viongozi waliopata
nafasi ya kuitumikia jamii kuhakikisha wanafuata maadili na kutanguliza hofu ya
mungu ili nchi iweze kufikia malengo yake.
Wito huo umetolewa juzi na Mchungaji Kiongozi,Thadeus
Ketto wakati
akitoa Salaam za mwaka mpya kwa waumini wake
ambapo alisema baada ya kuvuka salama 2021 mwaka 2022 ni mwaka wa matarajio makubwa na katika kuyafikia watanzania
wanapaswa kuanza na Mungu.
Ketto ambaye pia ni Mkuu wa jimbo la Pwani
alihimiza wananchi kufanya
kazi kwa bidii ili kujenga uchumi imara huku
akiwasisitiza vijana
kuchangamkia fursa katika kujiimarishia kipato.
"Nitoe wito kwa jamii kwa ujumla wake
tumtegemee Mungu zaidi,tufanye
kazi kwa bidii,vijana kuchangamkia fursa kama
bomba la mafuta tuwe
wanufaika wa kwanza,tutajenga uchumi wa
familia,jamii na nchi"alisema
Mchungaji huyo kiongozi Ketto.
Pamoja na hayo Ketto aliwasihi watanzania
kufuata sheria na taratibu
zilizowekwa nchini ikiwa ni kumuunga mkono Rais
Samia Suluhu Hassan
kumwezesha kutekeleza majukumu yake kwa mujibu
wa katiba.
Mbali na hayo Mchungaji Ketto amehimiza upendo
kwa kuhurumiana,kusaidia yatima,wanyonge
na wazee sanjari na utoaji wa elimu kwa jamii ikiwa ni miongoni mwa matendo yanayompendeza Mungu.
Kwa mujibu wa Mchungaji Keto, KKKT ni Kanisa
ambalo limekuwa na
ushirikiano mkubwa na Serikali kuhakikisha
linaifikia jamii katika
nyanja zote muhimu akitaja afya,elimu na hata
suala la uchumi.
Kwa upande wake KKKT imejipambanua kwa vitendo
kwa kujenga hospitali kama ile ya Bumbuli
wilayani Lushoto, Kilindi huku wakitoa michango Zahanati ya Mtimbwani jinni Tanga na Pwani.
Vilevile KKKT imekuwa na mchango mkubwa kwenye
sekta ya elimu ambapo imediriki kubeba
jukumu la kuwalipia ada wanafunzi na kwamba wanayo kamati inayohusika kusaidia wasiojiweza kama wazee.
Akizungumzia janga la UVIKO 19,alisema kwamba wameendelea
kutoa elimu kwa waumini,kuchukua
tahadhari na kuwakumbusha umuhimu wa kupata chanjo ya ugonjwa huo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment