Sunday, 2 January 2022

TIMU YA TANESCO MKOA WA TANGA SOKA IMEENDELEA KUONYESHA UBABE KWA WAPINZANI WAO KOMBANI PANGANI NA HALE KOROGWE,,

 



Pichani ni miongoni mwa wachezaji wa timu ya soka ya Tanesco mkoa wa Tanga mara baada ya mchezo wao wa kirafi dhi ya Tanesco Kombain ya Hale na Pangani wa kufunga mwaka. 

NA SOPHIA WAKATI,TANGA

MCHEZO wa Soka kusherekea kuingia kwa mwaka mpya kati ya Tanesco Tanga imeibamiza Kombaini ya Tanesco Pangani na Korogwe kwa magoli 2 - 1.

Katika mchezo huo uliofanyika uwanja wa Galanosi jijini Tanga magoli ya Tanesco mkoa wa Tanga yalifungwa na Ally Said dakika ya 23 katika kipindi cha kwanza cha mchezo.

Goli la pili la Tanesco Tanga lilifungwa na Mohamed Hassan dakika ya 49 huku wapinzani wao Kombaini ya Tanesco Kituo cha Pangani na Hale Korogwe nyumba ya Mungu wakiambulia goli moja la kufutia machozi kupitia Peter Mpina dakika ya 84.

Akizungumza baada ya mtanange huo,Nahodha wa Tanesco Tanga,Zuberi
Sebiga alisema kufanyika kwa mchezo huo kumewawezesha kuboresha
mahusiano mahali pa kazi.

Pamoja na hayo Seboga alisema michezo ni eneo muhimu ambalo mbali na kuboresha mahusiano lakini pia husaidia kujenga afya za wafanyakazi kupitia michezo.

Kwa upande wake Nahodha wa timu ya Tanesco Kombaini,Lwitiko Mwalusambo alielezea kuridhishwa kwake na matokeo waliyopata mchezoni huku akisema wanakwenda kujifua kwa mazoezi ili waweze kurejesha kipigo kwa wapinzani wao.
Mwisho.


No comments:

Post a Comment