Tuesday, 12 July 2022

KLABU YA COASTAL UNION YAWATOA HOFU MASHABIKI WAKE,,TUNA MIPANGO MINGI KUPATA HAZINA YA WACHEZAJI WAZURI,,,,

 
Pichani ni Kaimu katibu mkuu wa klabu ya Coastal Union,Jonathan Tito akizungumzia mpango mkakati uliopo ndani ya klabu ya Coastal Union.

 Kaimu katibu mkuu wa klabu ya Coastal Union,Jonathan Tito akizungumzia mpango mkakati uliopo. mpaka tunachukua maamuzi ya kutoa wachezaji kwenda kwenye vikosi vyengine tayari tumeshaanza taratibu za kufua wachezaji kuziba nafasi.

Amesema kwamba kufikia nafasi ya saba sio malengo yao msimu huu,ilikuwa ni kufika fainal na kuibuka kuwa bingwa kombe la Azam lakini baada ya kukamilika lengo moja kufika fainal ya kombe la Azam kushindwa kuchukua ubingwa tunajipanga upya kuja kivyengine,

Kuhusu wachezaji ambao wamekwenda vilabu mbalimbali tunajipanga kupata wachezaji wazuri zaidi kama kina Mamnyeto,Victa,Lyanga ilikuweza kushiriki msimu ujao.

Pia amesema msimu ujao wa ligi utakuwa wa mfano kwa klabu hiyo ya Coastal Union mbali ya kuwa na wachezaji wapya kwa kushirikiana na wale ambao walikwenda kwenye vilabu kwa mkopo watakuwa wamerudi kuitumikia klabu yao.

Pichani Kaimu katibu mkuu wa klabu ya Coastal Union,Jonathan Tito amewataka wanachama wa klabu hiyo kuendelea kuisapoti na kuimbea dua timu yao ili iweze kutimiza mipango yake na kufanya vizuri azidi msimu ujao.

No comments:

Post a Comment