Monday, 4 July 2022

Pichani mkono wa kulia ni Mgombea,Henry Daffa Shekifu jana akirunisha fomu ya kuwani kinyang'anyiro kutetea wadhifa wake wa Uenyekiti wa Chama tawala mkoani Tanga jana kwa katibu wa CCM  mkoa wa Tanga,Suleiman Mzee Suleiman (mkono wa kushoto) ofisini kwake. 



 NA SOPHIA WAKATI,TANGA

Henry Daffa Shekifu amejitokeza kuingia kwenye kinyang'anyiro kutetea wadhifa wake wa Uenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga.

Leo  (jana 3/07/2022) Shekifu ambaye amefanikiwa kuongoza kwa awamu mbili alichukua na kurejesha fomu hiyo ya kuomba kuwania Uenyekiti wa Chama tawala Mkoa huo.

Katika mazungumzo yake na Wanahabari, Shekifu alisema, anatetea nafasi yake hiyo ili kushirikiana vyema na watendaji waliopo katika kuyasimamia na kuendeleza yale waliyoanzisha kwa maslahi ya chama
tawala.

Aliwaeleza wanahabari kuwa tayari kuna miradi kadhaa waliyoanzisha lengo likiwa kukipa uhai wa kiuchumi chama cha mapinduzi ambayo inahitaji viongozi madhubuti katika kuisimamia.

"Ninyi wenyewe waandishi wa habari mnaweza kuwa mashahidi hata mkitizama kushoto kwenu mnaona jengo,haya ni mawazo tuliyoanzisha ili kusimamia uchumi wa chama,unahitajika uongozi madhubuti kuyasimamia haya"alisema Shekifu.

Katika maelezo yake hayo, Shekifu alijivunia mshikmano, uhusiano mzuri hata na vyama vya upinzani hatua ambayo anasema imesaidia kuwavuta wengi kurejea chama cha mapinduzi CCM.

"Siku zote tunashirikisha wapinzani kwenye viko vinavyohusu watu wote,mwenzako akikwambia jambo unajisahihisha,hawa wanasaidia na wametufikisha mbali"alisema Shekifu.

Aidha Shekifu alisema kwamba katika uongozi wake amesimamia nidhamu jambo ambalo limechangia upatikanaji viongozi vijana wengi kwa ngazi mbalimbali ikiwemo ile ya kitaifa.

Kutokana na hayo, Shekifu alisema amechukua fomu ili kuendelea kusimamia vizuri mambo yote yatakayozidi kuimarisha chama hicho kinachoendelea kushika dola.

"Tumesimamia vizuri nidhamu, tunataka tuwaachie hilo kama urithi wetu,hatuna ugonvi na upinzani tunajitetea kwa sera"alisema Shekifu huku akibainisha kuwa mawazo ya wapinzani yamekuwa yakiwasaidia kufanya marekebisho.

Zaidi ya yote Mwenyekiti huyo anayetetea wadhifa wake amesema,ndani ya uongozi wake wamefanikiwa kuondosha figisufigisu kwa watu kukatwa majina yao wanapokuwa wakiwanio nafasi mbalimbali za uongozi.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment