Monday, 4 July 2022

WAGOMBEA WAJITOKEZA KUWANIA NAFASI ZA UONGOZI OFISI YA CCM WILAYANI PANGANI.


Pichani mkono wa kushoto ni Mgombea Abdallah Mahamud Abdallah baada ya kuchukua na kurudisha fomu kwa katibu wa CCM wilaya ya Pangani,Zawad Nyambo (mkono wa kulia) kwa ajili ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani juzi.



Pichani aliyevaa sare ya CCM ni Mgombea Abdallah Mahamud Abdallah juzi kabla ya kuchukua fomu akisaini kitabu cha wageni ofisi ya CCM wilaya ya Pangani, kwa ajili ya kuwania nafasi ya Uenyekiti wa CCM wilaya ya Pangani.


Pichani ambaye amesimama ni Mkandarasi wa Kampuni ya Yajuk Investiment Co ltd ya Jijini Dar es salaam, Abdallah Mahamud Abdallah  mara baada ya kukabidhiwa mradi wa maji kijiji cha Mugobe na Kiloza wilayani Korogwe akizungumza na wananchi akiomba ushirikiano.


 NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE

WANANCHI wa kiloza Kata ya Magila Gereza iliyopo wilayani Korogwe mkoani Tanga,wanatarajia kuondokana na Kero ya upatikanaji wa huduma ya Maji baada ya ujenzi mradi unaogharimu shilingi million .700 za kitanzania utakapokamilika.

Kauli hiyo imetolewa na Mkandarasi wa Kampuni ya Yajuk Investiment Co ltd ya Jijini Dar es salaam, Abdallah Mahamud Abdallah alisema juzi mara baada ya kukabidhiwa mradi wa maji kijiji cha Mugobe na Kiloza wilayani Korogwe.

Katika mkutano huo wa kutambulishwa kwa wananchi wa Kiloza na kuomba ushirikiano ambapo alisema kuwa wamejipanga kukamilisha mradi huo kwa haraka ili kuondosha kero kwa jamii.

Mkandarasi Abdallah alisema kwamba tangu Mei 31 mwaka huu wamesaini mkataba wa kutekeleza mradi huo unaotarajiwa kumalizika  Novemba 31.mwaka huu.

Kwa mujibu wa mkandarasi huyo alieleza kazi zitafanyika usiku na mchana hatua ambayo lengo lake ni kufikisha maji haraka kwa wananchi.

Hata hivyo,Mkandarasi huyo alisema kuwa wakati wa utekelezaji ujenzi wa mradi huo kipaumbele cha ajira za Vibarua kitakuwa ni Vijana wa maeneo hayo.

Pamoja na hayo vijana hao wa Kiloza Magila Gereza wakikosa utayari wa kufanya kazi hizo Kampuni italazimika kutafuta Vibarua wengine hatua ambayo itawawezesha kukamilisha ujenzi wa mradi kwa wakati.

Nae Diwani wa kata ya Magila Gereza,Mwajuma Kitumpa alisema iwapo mradi huo utakamilika utapunguza adha waliyoipata wanawake hapo awali.

Aidha,alisema kwamba wanawake hapo awali walilazimika kutembea umbali mrefu kupata huduma ya maji jambo ambalo liliwakwaza kutekeleza majukumu mengine.

Diwani Mwajuma aliwasihi wananchi wake kushirikiana vyema na mkandarasi wakati mradi utakapoanza kutekelezwa huku akibainisha kuwa hakutakuwa na fidia yoyote.

Kwa upande wao miongoni mwa wananchi wa Kiloza,Bakari Chanyegela wameonesha kuridhishwa kwao kwa upatikanaji mradi huo wakiahidi kumpatia mkandarasi ushirikiano.

Vilevile wamesema akitokea miongoni mwao kupinga uwepo wa mradi huo watalazimika kuchukua hatua ya kumtenga kwa vile maji ni kero ya muda mrefu na sasa imepata ufumbuzi.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment