Wednesday, 28 September 2022

DIWANI KATA YA DUGA AMEISHUKURU SERIKAL MITAA YAKE 14 KUNUFAIKA NA MPANGO WA TASAF,,,

 




Pichani ni Diwani kata ya Duga halmashauri ya jiji la Tanga,Jafari Mohamed akiishukuru halmashauri na serikali juu ya kata yake yenye mitaa kumi na nne yote ilivyonufaika baada ya kufikiwa na mpango wa Tasaf kuhudumia kaya masikini.






Wanufaika wa mpango wa TASAF halmashauri ya jiji la Tanga wakiwa nje ya ofisi ya mtendaji kata ya Duga wakisubiri utaratibu wa kupokea fedha.

Pichani mwanamke ambaye amesimama mkono wa kushoto ni Mwezeshaji wa TASAF Kata ya Duga  halmashauri ya jiji la Tanga, Farida Hatim akitoa elimu kwa vijana kwamba mpango huo utahusisha walengwa wa moja kwa moja,walioteuliwa ndani ya kaya kuanzia miaka 18 hadi 65 watahusika.


Pichani ni baadhi ya vijana wakiwa wametumia kukaa chini ofisi ya mtendaji kata ya Duga wakimfuatilia mwezeshaji.

NA SOPHIA WAKATI,TANGA
MPANGO wa Tasaf kuhudumia Kaya masikini umeendelea kujiimarisha ambapo sasa walengwa watahusika kufanya ajira za muda na hivyo kumudu kujiimarisha kiuchumi.

Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji wa TASAF Kata ya Duga, Farida Hatim alisema juzi kuwa,mpango huo utahusisha walengwa wa moja kwa moja,walioteuliwa ndani ya kaya kuanzia miaka 18 hadi 65 watahusika.

Alisema kwamba tayari shughuli za uibuaji miradi zimefanyika walengwa na wananchi wengine wakishirikishwa kuhusu miradi hiyo ya kijamii katika maeneo yao.

Hata hivyo,Hatim alisema, wanawake wajawazito na wanaonyonyesha hawatahusika kwenye ajira hizo ambapo  watashiriki watakapomaliza miaka miwili ya kunyonyesha.

Vilevile,alibainisha kuwa wanaotoka nje ya kaya za walengwa na wanafunzi hawatahusika katika ajira hizo za muda akitolea mfano wa kazi hizo za muda kuwa ni uchimbaji wa mifereji na nyinginezo.

Naye Diwani wa kata ya Duga,Japhari Mohamed alisema kata yake yenye mitaa kumi na nne yote imenufaika baada ya kufikiwa na mpango wa Tasaf kuhudumia kaya masikini.

Aliishukuru serikali ya awamu ya sita kwa jitihada zake za kuwakwamua wanyonge akisema wengi wa wananchi wake hivi sasa uchumi wao umeimarika.

"Kiukweli wananchi wangu wamefikia hali nzuri hata kufikia kujengewa nyumba kwa mpango wa tasaf,tuna walengwa 381"alisema Jafari.

Mwenyekiti wa mtaa wa Mapinduzi,Athumani Mganga ametumia nafasi hiyo ameomba wazee kuwekewa utaratibu maalum kupokea ruzuku zao kwa maelezo kuwa wamekuwa wakipata changamoto kutoka kwa mawakala.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment