Wednesday, 28 September 2022

CCM KOROGWE MJINI YAWAASA WANACHAMA WANAOWANIA UONGOZI KUFUATA MIIKO YA UCHAGUZI,,,


 


Pichani KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Korogwe Mjini,Evarist Mluge kuelekea uchaguzi akiwaasa Wanachama wanaowania Uongozi kuheshimu taratibu na miiko ya uchaguzi huku akieleza kwamba
atakayebainika kukiuka hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
 

NA SOPHIA WAKATI,KOROGWE
CHAMA Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Korogwe Mjini, kimewaasa Wanachama wanaowania Uongozi kuheshimu taratibu na miiko ya uchaguzi na kwamba
atakayebainika kukiuka hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.

Katibu wa Chama hicho tawala Wilayani humo, Evarist Mluge alitoa rai hiyo juzi Ofisini kwake huku akisema, wote waliochukuwa fomu kuwania uongozi wa chama na jumuiya wanapaswa kuheshimu taratibu na miiko ya
uchaguzi wa CCM.

Mluge alisema,kwamba wanachama waliochukua fomu, hawatakiwi kujihusisha na Kampeni chafu kama kujipitisha kwa wapiga kura na hata kutoa takrima
mambo ambayo alisema ni kinyume na taratibu.

Aidha,alibainisha kueleza kwamba,mwanaCCM atakayebainika kuhusika na vitendo hivyo ambavyo ni kinyume na maadili  atachukuliwa hatua za kinidhamu likiwemo suala la jina lake kutopendekezwa.

"T\Wanachama tufuate kanuni na taratibu zilizopo ndani ya CCM,atakayebainika kukiuka hatua za kinidhamu zitachukuliwa mbali na kuenguliwa jina lake hatua nyingine zitafuata"alisema Mluge.

Katibu huyo,Mluge alisisitiza umuhimu wa wagombea hao kuheshimu taratibu ili uchaguzi kuweza kumalizika kwa usalama hatua ambayo pia itaepusha kujitokeza kwa mipasuko ndani ya chama.

Alisema kuwa, ngazi zote za chini safu za uongozi zimekamilika, mchakato unaoendelea ni wa ngazi ya wilaya ulioanza Julai kwa wanachama wote kuchukua fomu.

Aliendelea kusema kuwa,tarehe 16 na 17 mwezi huu ni uchujaji majina kwa ngazi ya wilaya na kwamba kanuni na taratibu za uchaguzi zinaelekeza kuwa nafasi zote zinafanyiwa uteuzi na vikao vya halmashauri kuu ya mkoa.

Nafasi hizo ni wajumbe halmashauri kuu wilaya,makatibu siasa na uenezi,wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa na wajumbe wa mkutano mkuu Taifa isipokuwa nafasi ya Mwenyekiti wilaya itajadiliwa ngazi ya Taifa kupitia kamati kuu.

Katibu huyo wa CCM Korogwe Mji (Mluge) amewasihi wanaCCM kuendelea kufanya subira wakati taratibu za msingi zikiendelea kuelekea uchaguzi huo kuhitimishwa.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment