Waziri,Aweso akizindua bodi ya tisa (9) ya Maji ya TANGA UWASA,
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WAZIRI wa Maji,Jumaa Aweso ameiagiza bodi mpya ya Tanga UWASA kuhakikisha inafikisha huduma maeneo ya pembezoni na kushughulikia malalamiko ya wateja wao likiwemo suala la wananchi kubambikiwa ankara za Maji.
Aweso ameyasema wakati akizindua bodi ya tisa (9) ya Maji, huku akisema baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumwamini wadhifa huo amesema hatakuwa kikwazo kwa Watanzania na Wananchi wa Tanga kupata huduma ya maji.
Alisema, kwamba walioingia kwenye bodi mpya wamepewa dhamana kubwa ya kuhakikisha Mamla ya Maji Tanga UWASA inakwenda vizuri kiutendaji ikiwemo kuboresha huduma ya maji kwa jamii.
Alisema hadi kufikia 2023 Mamlaka hiyo inatakiwa kufikisha maji vijijini kwa asilimia 85 huku mjini ikiwa asilimia 95 akieleza kuwa kazi iliyopo kwa bodi mpya ni kufikisha maji maeneo ya pembezoni.
"Wajumbe wa bodi mna kazi kubwa ya kufanya hadi pembezoni mhakikishe mnafikisha huduma,mshughulikie malalamiko,watu wasibambikiziwe bili,kwa sasa tuna asilimia 96 ya utekelezaji huduma,mtu akiomba huduma apate ndani ya siku saba"alisema Aweso.
Aidha,Waziri huyo wa maji alisema, miradi mingi ya maji imekamilika kwa wakati hivyo amewataka wahusika kufanya uzinduzi ili kutoa fursa kwa wananchi kupata huduma stahiki kupitia serikal.
Pamoja na hayo,Pia Waziri Aweso alitumia nafasi hiyo kuwataka watendaji kuendelea kufanya kazi zao kwa bidii huku akitanabaisha kuwa Wakandarasi wababaishaji hawataweza kufumbiwa macho.
"Mkuu wa mkoa wa Tanga Mgumba namwelewa ni mchapakazi,awakalie kooni wakandarasi wa maji wababaishaji ili watafute shughuli ya kufanya,anayefanya kazi apewe ushirikiano asiyefanya ataondolewa"alisema.
Aidha,alibainisha kuwa bodi ya nane iliyomaliza muda wake imefanya kazi kubwa na ile iliyoingia madarakani inapaswa kukamilisha viporo vilivyoachwa na kuanzisha miradi mipya ili kuacha alama ya utendaji.
Pia Waziri Aweso amesisitiza kusema kuwa wahandisi wa maji wanatakiwa kufuatilia miradi badala ya kungoja viongozi huku akiwasihi maafisa utumishi kufuatilia maslahi ya wafanyakazi.
Kwa upande wake miongoni mwa wajumbe wa bodi waliomaliza muda wake,Mustapher Selebos alisema wamefanya mambo makubwa huku akiishukuru Wizara kwa kuwapatia miradi mingi.
Alisema katika fedha zote walizopokea thamani imezingatiwa kwenye miradi huku akieleza kwamba mamlaka imekuwa ikishiriki kusaidia jamii kwenye sekta ya afya,elimu na hata michezo.
Hata hivyo,alisema wanakabiliwa na changamoto nyingi huku akitaja kubwa kuwa ni uwepo wa chanzo kimoja cha maji ambapo wameshatayarisha andiko ili kufanyiwa ukarabati.
Mwisho.

No comments:
Post a Comment