Thursday, 6 October 2022

UCHAGUZI WA KUMPATA MWENYEKITI WA CCM WILAYANI PANGANI MWAKA 2022 ULIKUWA HIVI,,,

Pichani ambaye amesimama ameshika kipaza sauti ni Abdallah Mahmoud mara baada ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani kwa kupata kura 411 huku akiwagaragaza wapinzani wake wawili waliokuwa wakiwania kiti hicho,akiwashukuru wanachama kwa kumchagua na kueleza vipaumbele vyake katika utendaji.

Pichani katikati ni Mwenyekiti mpya wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Pangani,Abdallah Mahmoud baada ya kuchaguliwa akisalimiana na aliyekuwa mwenyekiti  wilayani hapo,Rajabu Abdurahamani akimpongeza kwa ushindi huo.


Pichani wa kwanza mkono wa kulia ni Mbunge wa jimbo la Pangani,Jumaa Aweso akifuatiwa na Katibu wa CCM wilaya ya Pangani,Zawadi Nyambo.

 NA SOPHIA WAKATI,PANGANI

KADA Abdallah Mahmoud amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Pangani kwa kupata kura 411 huku akiwagaragaza wapinzani wake wawili waliokuwa wakiwania kiti hicho.

Akitangaza matokeo ya Uchaguzi huo juzi Msimamizi wa,Salim Mohamed Ratco ulifanyika kwenye ukumbi wa YMC wilayani hapa ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM taifa, alisema katika uchaguzi huo kulikuwa na wagombea watatu ambapo alisema kati ya kura 447 zilizopigwa mbili ziliharibika.

Aliwataja wagombea wengine kuwa  ni Omari Ally aliyepata kura( 5) na Shafii Akida ambaye aliambulia kura (29 ) katika kinyang'anyiro hicho.

Aidha pia Msimamizi huyo wa uchaguzi aliwatangaza washindi katika nafasi za wajumbe wa mkutano mkuu wa Taifa kutoka wilaya ya Pangani ni John Semkande kura 155,Mfaume Omari kura 210,Fatuma Suleman kura 229.

Alisema kwamba katika uchaguzi huo kura halali 434 kati ya awali 465 huku kura 31 zikiharibika na hivyo halisi kubakia 403.

Aliwataja wagombea ambao walibwagwa katika kinyang'aro hicho kuwa  ni Seif Ally Said (135),Salim Ally (123),Amina Abdallah (120),Saumu Mbaruku (99),Seleman Rashid (84) na Omari Iddi (55).

Alisema pia katika uchaguzi huo walipatikana wajumbe  wawili wa nafasi ya Mkutano Mkuu wa Mkoa ambapo kura zilizopigwa  445 zilizoharibika ni 47 hivyo kufanya kura halisi kuwa 398.

Aliwataja wajumbe hao wawili ambao ulikuwa na wagombea sita kuwa ni Rajabu Omari (160) na Fatuma Seif (223) huku wakiwabwaga wapinzania Omari Rahim(63),Mbwana Andrew(92).

Aidha kwa upande wa nafasi kundi la wakina Mama nafasi 4 ambazo zilikuwa zikiwaniwa na wagombea  watano ambao walioshinda ni Mwana hasani Omari kura (204),Aisha Abdul (201),Amina Abdallah(195) na Amina Mohamed Salehe (192) huku Mwanahara Omari akigaragazwa kwenye kinyangany'iro hicho kwa kupata kura (95).

Katika uchaguzi huo kura zilizopigwa zilikuwa 449 kati ya hizo 19 zikiharibika huku 430 zikiwa ni kura halali.

Hata hivyo Msimamizi huyo alisema kwamba katika nafasi ya kundi la wazazi watakaokwenda kuwakilisha wilaya hiyo kwenye Halmashauri Kuu Mkoa wa Tanga kuwa ni Twalibu Omari(216) na Salmini Abdi Omari(164) huku wakiwabwaga wapinzani wao Omari Zuberi (83),Ally Sima (53),Rajabu Msomali (140),Shomari (142).
Mwisho

No comments:

Post a Comment