Monday, 21 November 2022

TAREMA INA MPANGO MKAKATI KUTOA ELIMU KWA WACHIMBAJI ILI KUHESHIMU MAENEO YENYE VYANZO VYA MAJI,,,,



Pichani ni Mwenyekiti wa TAREMA, Iddi Mhina akieleza mpango mkaka wa kufungua ofisi halmashauri ya Bumburi na Lushoto ili kurahisisha shunguli za uchimbaji madini.


NA SOPHIA WAKATI,LUSHOTO
 CHAMA Cha Wachimba Madini Mkoani Tanga kimejipanga kutoa elimu kwa Wadau wake ili kudhibiti na kuwaondosha bila kutumia nguvu Kwa watakaodiriki kuendesha uchimbaji kwenye vyanzo vya maji.


Mwenyekiti huyo wa TAREMA, Iddi Mhina alitoa taarifa hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari wilayani Lushoto mpango mkakati uliopo kwa wachimbaji.

Katika mazungumzo yake hayo,Mhina alisema kuwa ameanza ziara katika wilaya hizo lengo kukutana na wadau maeneo mbalimbali ya mkoani Tanga.

Alisema kwamba tayari amefanya kikao na wadau wakiwemo madiwani wa Lushoto mjini na Bumburi kwa maana ya wachimbaji.

Aidha,alisema kuwa katika ziara yake hiyo amebaini uwepo wa wachimbaji wa kutosha Jimbo la Bumbuli lenye madini ya Boxite ambapo kumewekwa mkakati.

Hata hivyo,Mhina alisema kwa madini hayo ya Boxite wamefikia hatua za mwisho kuwawezesha kupata kibali ili eneo la Magamba uchimbaji uweze kufanyika.

"NEMC katika taarifa yao ya awali wamesema Boxite inaweza kuchimbwa na imeonekana kutokuwa na madhara kwa binadamu pia hakutakuwa na athari kubwa kwa mazingira" alisema Mhina.

Licha ya kuyasema hayo,Mhina pia ametumia nafasi hiyo amewataka wananchi kuwa watulivu wakati michakato stahiki ikiendelea kufanyiwa kazi.

Kwa mujibu wa Mhina kwa sasa utaratibu unaoendelea ni ule wa kuwabaini wachimbaji wenye leseni na wasiokuwa nazo kupitia 'data base' ya chama cha madini na kwamba kule kusiko na viongozi walisimikwa viongozi wa muda kabla ya uchaguzi kufanyika.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment