Pichani katikati mwanamke ambaye ameshika kipaza sauti ni Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Tanga, Zainabu Bakari akiwawahutubia wanavyuo vya juu na kati,akiwataka kushirikiana kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya rushwa za ngono vyuoni huku akibainisha kueleza Kongamano la mwaka 2022 wametumia kufanya shughuli mbalimbali kwa jamii katika wilaya zote za mkoa huo ikiwemo kutoa elimu kwenye makundi.
Pichani ni baadhi ya washiriki wa kongamano lililoandaliwa na TAKUKURU mkoani Tanga,wadau klabu za wapinga rushwa,walimu na wanavyuo vya juu na kati wakiwasikiliza viongozi wakiwahutubia.
Pichani mkono wa kushoto ni mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Tanga,Hashim Mgandilwa ambaye amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Tanga,Omari Mgumba mara baada ya kufungua kongamano hilo akisindikizwa na kamanda wa TAKUKURU mkoa huo (katikati) na mkuu wa dawati la habari mkoa Frenk Mapunda(mkono wa kulia na viongonzi wa wilaya zote za mkoa wa Tanga.
Pichani ni mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Tanga,Hashim Mgandilwa akiteta kitu na Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Tanga,Zainabu Bakari kabla ya kufungua kongamano hilo.
Pichani kushoto ni mgeni rasmi akiteta jambo na kamanda wa TAKUKURU maafisa wa wilaya zote za mkoa wa Tanga na msajili wa chuo cha veta Tangaambaye amevaa shati jeupe.
Pichani ni maafisa wa TAKUKURU mkoa wa Tanga,wilaya na wadau na klabu za wapinga rushwa mkoani hapo wakiwa kwenye kongamano hilo ambalo wamelitumia kupinga vitendo vya rushwa ya ngoni vyuoni.
Pichani ambaye ameshika kipaza sauti ni mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Tanga, Hashim Mgandilwa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Tanga,akiwataka wanavyuo vya juu na kati akiwahimiza kuona umuhimu wa mafunzo yanayotolewa na TAKUKURU ili kuweza kutimiza ndoto zao za baadaye,mkono wa kulia ni kamanda wa Takukuru mkoani Tanga,Zainabu Bakari.
NA SOPHIA WAKATI,TANGA
WANAFUNZI wa Chuo cha Mafunzo ya ufundi stadi Veta Jijini Tanga wamesema, licha ya uwepo wa rushwa ya ngono miongoni mwa jamii,wanaungana na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na rais Samia Suluhu Hassan katika kupambana na vitendo hivyo.
Kauli hiyo imetolewa na Mwanachuo wa fani ya ufundi bomba chuo cha Veta, Mwanakombo Mnyeto aliyasema hayo alipohudhuria Kongamano la kupinga rushwa ya lililofanyika mwaka huu 2022 chuo cha Veta kilichopo jijini Tanga.
Katika Kongamano hilo lililoandaliwa na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU mkoani Tanga, wanachuo hao walionesha uelewa wa kukiri uwepo wa rushwa ya ngono kwa jamii huku wakiapa kupambana nayo.
"Tumeelimika tunapinga rushwa ikiwemo ya ngono, tunajua ipo ila hapa chuo cha Veta hakuna,tunaungana na Serikali kuikomesha kwa vile ina athari kubwa kwa watoto na vijana" walisema.
Mwanakombo aliyataja moja ya madhara ya rushwa ya ngono kwa wanafunzi kuwa ni pamoja kushindwa kutimiza ndoto zao kwa baadhi kupata magonjwa ya kingono na changamoto nyingine.
Naye Mwanafunzi,Oscar James anayesomea ufundi bomba ambaye ni Waziri wa serikali ya wanafunzi Veta jijini Tanga alisema, elimu wanayopatiwa mara kwa mara imewasaidia wengi katika kumudu kutimiza ndoto zao.
Kamanda wa TAKUKURU Mkoani Tanga, Zainabu Bakari alisema kuwa mwaka huu wametumia maadhimisho hayo kwa kufanya shughuli mbalimbali kwa jamii ikiwemo kutoa elimu kwa jamii, vyuo vya kati na vile vya juu.
Alisema,lengo la kongamano hilo kwa wanafunzi alisema kundi la wanachuo ni tegemeo la ustawi wa Taifa wakati wanapoelekea kazini, hivyo wanapopatiwa elimu inasaidia kupunguza kama si kumaliza kabisa tatizo la rushwa.
''Katika maadhimisho ya mwaka huu tumeanza chini kwenye wilaya zote za mkoa wa Tanga kushiriki shughuli mbalimbali kabla ya kongamano hili la mkusanyiko wa pamoja Jijini Tanga''alisema Zainabu.
Hata hivyo alisema, Takukuru inahitaji ushirikiano ili kufanikiwa kuliondoa Taifa kwenye rushwa,pia amebaishanisha kwamba mapambano yanaendelea kutokomezavitendo vya rushwa ikiwemo ya ngono.
Alisema la kongamano hilo kwenye vyuo vya juu na kati ni kuwakumbusha athari inayotokana na vitendo vya rushwa ili kujiepusha na kuona umuhimu wa kujikita kwenye elimu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mkuu wa wilaya hiyo Hashim Mgandilwa, amehimiza umuhimu wa Takukuru kushuka chini zaidi ili kuwajengea uwezo watoto na kuwawezesha kujitambua hatua itakayosaidia kupata watumishi wazuri ya baadaye.
Pia amewataka vijana kuona umuhimu kutumia mafunzo wanayopata ili kuweza kubadilika huku akiwahimiza wanafunzi kujikita zaidi kwenye masomo yao.
Mwisho.
Pichani ni miongoni mwa WanaChuo cha Mafunzo ya ufundi stadi Veta Jijini Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi,msajili wa chuo cha Veta na kamanda wa Takukuru mkoa wa Tanga na viongozi wa Takukuru wilaya mbalimbali wa mkoa za Tanga.
No comments:
Post a Comment