Pichani ambaye ameshika kipaza sauti ni Mwenyekiti wa CCM Mkoani Tanga,Rajabu Abdurahaman akieleza kusikitishwa kwake na DMO Pangani kuchelewa utekelezaji nyumba ya mganga zahanati ya Ushongo.
NA SOPHIA WAKATI, PANGANI
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdurahman ameelezea kusikitishwa kwake na kitendo cha Mganga Mkuu wa Wilaya ya Pangani kushindwa kusimamia kikamilifu Ujenzi wa nyumba ya Mganga Zahanati ya Ushongo ili kukamilika kwa wakati.
Abdurahman ameyaeleza hayo jana, wakati alipofanya ziara yake Mwera wilayani humo ambapo alipata fursa ya kutembelea Ujenzi Nyumba ya Mganga Zahanati ya Ushongo, ambapo Zahanati ilijengwa kwa nguvu za Wananchi huku Serikali ikiwa imetoa Milioni 150 kujenga nyumba hiyo.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti huyo, licha ya fedha hizo kutolewa tangu Mwezi Februari Mwaka huu, ujenzi huo umeonekana ukizorota na kuendelea kusababisha kero kwa Wananchi ambao wamekuwa wakitumia gharama kubwa za Usafiri kwenda Mwera kupata matibabu.
“ Milioni 150 mmepewa tangu ,mwezi wa pili zilipoletwa ila hamkutekeleza chochote, Pangani inaonekana imeota miziz kwa tabia za namna hii na sisi hatutakubali Chama kikaadhibiwa kwa ajili ya uwepo wa Watumishi aliowaita kuwa wazembe” alisema Mwenyekiti huyo.
Pia amemtaka Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani,Isaya Mbenje kuchukua hatuia katika mradi huo katika kipindi ambacho Wananchi wameshaweza kuchukua hatua ya kuchangia nguvu kazi.
“DMO nimekutetea sana Tangu nikiwa Mwenyekiti wa CCM wilaya hii lakini hukuweza kujirekebisha, sasa hatuwezi kwenda na Watumishi wa aina hii” alisema Mwenyekiti wa CCM Mkoa huku akiahidi kurejea tena kuona ujenzi wa nyumba unavyoendelea baada ya miezi mitatu.
Awali katika taarifa yake kwa Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Tanga, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Pangani,Maulidi Majala alisema kwamba, wamepokea fedha ikiwemo Shilingi Milioni 150 kutoka Serikalini ili kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo nyumba hiyo Mganga Ushongo.
Kauli hiyo ya DMO ndiyo ilionekana kumkera Mwenyekiti wa CCM hatua ambayo ilimsababisha kutoa maelekezo hayo baada ya kubaini kuwa fedha zimetolewa muda mrefu na zimeshindwa kufanya kazi.
Mbunge wa Jimbo la Pangani ambaye pia ni Waziri wa Maji, Jumaa Awesso alisema, baada ya kuona Wananchi wameanza kutumia nguvu zao kujenga Zahanati hiyo ndipo alipochukua hatua ya kuomba fedha Serikali ambapo walipatiwa Shilingi 150 zilizotolewa mwezi Februari.
“Katika ziara zangu nilipoona Wananchi wamejenga Zahanati kwa nguvu zao nilimwendea Rais kumuomba fedha na tukapata Milioni 150 Pangani ili kujenga nyumba ya Mganga lakini mpaka leo hakuna kinachofanyika” alisema Mbunge Awesso huku akieleza kuwa DMO amewakosea sana Wananchi wa Pangani.
Aliongeza kusema:”Kwa hali hii hatuwezi kwenda, wataalam kwa hatua hii haiwezekani, DC tunaomba uchukue hatua” alisema Mbunghe huyo wa Chama Cha Mapnduzi CCM wilaya ya Pangani.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment