Thursday, 22 December 2022

KAMANDA TANGA,MWAIBAMBE AELEZEA JINSI POLISI WALIVYOFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WANNE WA FAMILIA MOJA KWA TUHUMA ZA KUMUUA NDUGU YAO KWA MGOGORO WA MPAKA WA SHAMBA,,


Pichani (ambaye amevaa kofia nyeusi) ni Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga,Henry Mwaibambe akieleza jinsi walivyofanikiwa kuwakamata ndugu wanne wa familia moja kwa tuhuma za 

NA SOPHIA WAKATI, LUSHOTO
WATU wa nne (4)  wa familia moja wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tanga,wakituhumiwa kumuua ndugu yao Ally Zayumba (52) mkazi wa Kijiji cha Sunga Wilayani Lushoto kwa ajili ya mgogoro wa aridhi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Tanga,Henry Mwaibambe, alisema juzi kuwa tukio hilo lilitokea Novemba 11,mwaka huu saa 3;00 usiku katika kijiji cha Sunga kilichopo tarafa ya Mtae wilayani Lushoto.

Alisema kwamba watuhumiwa hao wa Marehemu Ally ambao ni ndugu zake walimvizia wakati akitoka matembezi ambapo walimpiga na kitu kizito kichwani hadi akapasuka na kutokwa na damu nyingi.

Alieleza kuwa Marehemu Ally baada ya shambulio alianguka chini na ndipo watuhumiwa walipoukunja mwili wake na kuufunga kwenye Chandarua na kwenda kumtupa kwenye Msitu wa Shagai.

'Baada ya kufanya tukio hilo la mauaji ya ndugu yao watuhumiwa wote walitoeka kusikojulika na awali kabla ya tukio hilo baadhi ya ndugu walitoa taarifa za kupotea kwa Ally Zayumba''Alisema Kamanda Mwaibambe. 

Alisema mpaka sasa watuhumiwa wote wanne (4) wamekamatwa na taratibu za uchungunguzi zikikamilika watafikishwa Mahakamani kujibu Mashtaka yanayowakabili.

Kamanda huyo wa Polisi,Mwaibambe alisema baada ya taarifa hiyo ndipo polisi walianza msako maeneo mbalimbali kufanikisha kuwanasa.

Ndugu Wanaoshikiliwa na jeshi la Polisi kuhusiana na tukio hilo ni Omari Zayumba (25), ambaye ni fundi magari na mkazi wa Dar es Salaam na Saidi Zayumba (40) Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam.

Wengine ni Rajabu Zayumba (32) Mfanyabiashara na Mkazi wa Dar es Salaam na Muhuzar Hashimu maarufu'Mboga' (42) mkazi wa Kijiji cha Sunga.

Kamanda Mwaibambe alisema, watuhumiwa hao walikamatwa kutokana na Mauaji hayo yaliyotokea 14/11/2022 huko kwenye Kijiji cha Sunga, Mtae wilayani Lushoto.

''Mnamo 19/11/2022 ndgugu wa Marehemu walikwenda kituo cha Polisi Lushoto kutoa taarifa za kupotea kwa ndgugu yao ambapo Jarada la Uchunguzi lilifunguliwa na kufanikiwa kumkamata Omari Zayumba (25) aliyekiri kumuua Marehemu akiwa na wenzake watatu na kuwafuatilia''Alisema Mwaibambe.

Baada ya msako huo kufanyika wahusika wote waliweza kutiwa nguvuni katika mahojiano kukiri na kwenda kuonesha sehemu mwili wa marehemu ulipotupwa.

Kwa mujibu wa Kamanda polisi mkoa wa Tanga,Mwaibambe alibainisha kwamba mwili huo ulitupwa kwenye msitu wa Shaghai uliopo Kijiji cha Sunga wilayani Lushoto.

Polisi pia katika mahojiano na watuhumiwa walieleza chanzo cha kifo ni mgogoro wa ardhi waliyoipata kwa kugawana urithi baada ya kifo cha Baba yao.

''Eneo hilo la ardhi tayari walishagawana vipande vipande na marehemu anadaiwa kupanda michongoma eneo lake la mpaka ambayo hata hivyo inadaiwa kung'olewa na watuhumiwa''Alisema Kamanda Mwaibambe.

Kamanda Mwaibambe alisema kuwa mwili wa marehemu baada ya kukamilisha taarifa zao ulikabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya taratibu za mazishi ambapo hata hivyo ulikutwa ukiwa umeharibika vibaya.
Mwisho.

 




No comments:

Post a Comment